19 December 2014

Rais wa nchi ya Uruguay, Jose Mujica Akiwa nje ya Nyumba yake

Uruguay, imewapokea wafungwa wote wasio na hatia ambao walikuwa Guantanamo ambao wamekuwa wakiteswa kwa miaka bila ushahidi.

Wakati Mataifa yote Duniani, yakiwemo Mataifa ya Kiarabu yakiogopa kuwapokea watuhumiwa wasio na hatia, waliokuwa wamefungwa uko Guantánamo Bay,

Rais wa nchi ya Uruguay, Jose Mujica amekubali kuwapokea Wafungwa sita kutoka  Guantánamo Bay.

Watuhumiwa hao wanne wana asili ya Syria, mmoja Tunisia na mwingine Palestina.

Rais Jose Mujica, ambaye amejipangia mshahara wa dola $ 300 tu kwa wiki. Na anamiliki gari kuukuu aina ya Beetle yenye umri wa miaka 27, anaishi kwenye nyumba ya kawaida sana kulinganisha na mazoea ya marais wote walio madarakani.

 
Rais Jose Mujica akishuka kwenye Usafiri wake 

Ndege ya Kimarekani iliwapeka watuhumiwa hao uku wakiwa wamefungwa minyororo miguuni na pingu mikononi na uku wakiwa wamezibwa kwa vitambaa usoni.
Walipowasili tu Uruguay, Rais Mujica (ambaye yeye mwenyewe aliwahi kuteswa kwa miaka 13 chini ya utawala uliopita wa kidikteta) alisisitiza kwamba watuhumiwa hao wanapaswa kushushwa  wakiwa hawajafungwa pingu wala minyororo miguuni na waondolewe vitambaa walivyozibwa navyo usoni.

Waislam hao walilakiwa na kundi la raiya wa Uruguay uku wakikumbatiwa kwa furaha, kisha wakaongozwa kwenye nyumba walizo tayarishiwa kuishi.


Waislam hao wamepewa uhakika wa kupatiwa kazi na kulipwa mishahara kama raiya wengine wa Uruguay ili waanze maisha mapya wakiwa huru.

Hakuishia hapo tu, vilevile amewataka Waislam hao walete familia zao ili kuja kuishi nao nchini Uruguay, bila masharti yoyote yale. Na angaongeza kwa kusema kuwa wapo huru kuchaguwa timu watakayoipenda kuishabikia.

Uruguay ni nchi yenye idadi ya raiya wasiopungua milioni 3.3 na idadi ya Waislam wanao kisiwa kufikia mia tatu (300) tu.

----

Qur'an 94:5-6
Fa-inna maAAa alAAusri yusra
Basi kwa hakika pamoja na uzito upo wepesi,
Inna maAAa alAAusri yusra
Hakika pamoja na uzito upo wepesi.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!