3 June 2014

Wanaume ambao sio wanariadha wanasema maziwa ya Matiti yanawapa afya nzuri.
Baadhi ya wanaume wanasema maziwa ya Matiti inawapa nguvu za ajabu

 Wanariadha wanaume wamekiri kuanza kunywa maziwa ya Matiti kama njia ya kusisimua misuli yao badala ya kutumia madawa yaliyoharamishwa ambayo yanaongeza nguvu mwili.

Kwa mujibu wa jarida la Mail kwenye mtandao , wanyanyua uzani wengi wameanza kutumia maziwa ya matiti kama njia ya kujipatia nguvu.

Mwanariadha mmoja kutoka mjini New York kwa jina Antony, aliambia jarida la NYMag.com kwamba hukutana na wanariadha kadhaa ambao hunywa maziwa hayo ambayo wanasema ni mazuri na yanawapa nguvu.

Maziwa haya hununuliwa kwenye maduka ya mitandaoni ikiwemo mtandao ujulikanao kama 'Only the Breast and Human Milk 4 Human Babies' kwa dola mbini na nusu.

Mwanariadha huyo anasema kuwa maziwa hayo humpa nguvu za ajabu.

Sababu ya wao kufanya hivyo , ni kujizuia kutumia madawa ambayo yamepigwa marufuku kwani wanaamini kuwa maziwa ya Matiti ni njia ya kiasili ya kuwapa nguvu.

Mwanariadha mmoja ambaye ni baba wa watoto wanne Jason Nash, anasema alianza kunywa maziwa ya mkewe baada ya mtoto wao wa kwanza kuzaliwa na akahisi kuwa ikiwa maziwa hayo ni mazuri kwa mtoto basi pia ni mazuri kwa watu wazima.

Ananukuliwa akisema kuwa maziwa hayo yamemlinda kutokana na magonjwa miaka hii yote.
Wanaume kadhaa wamezungumzia kunywa maziwa ya Matiti kama njia ya kuwapa nguvu badala ya kutumia madawa ya kusisimua misuli.

Akijibu wakosoaji wake, wanaosema kuwa ni kitu cha ajabu na kushangaza, Antony alisema,'' mimi siamini madawa ya kusisimua misuli na ninataka vitu vya asili, ambavyo havina athari zozote mbaya kwa mwili.''

Wanaume wengine ambao sio wanaridaha ingawa wanakunywa maziwa ya Matit, wanasema kuwa maziwa hayo huwafanya kujisikia kama walio na nguvu mno na wenye afya tele.

David,mwenye umri wa miaka 42, kutoka Brooklyn, aliambia jarida hilo kuwa alianza kunywa maziwa ya matiti miaka mitatu iliyopita. Alisema ilisaidia sana wakati alipokuwa anapokea matibabu ya Saratani kwa kuwa alikuwa anahisi kutapika wakati wote alipokuwa anapokea matibabu.

Pindi alipokunywa maziwa hayo hisia za kutapika wakati wote zilimtoka. Alisema maziwa hayo ambayo ni matamu , yalimsaidia sana.


Sporce: http://nymag.com/
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!