27 January 2014


Kunguru na shakwe (seagull) wamewashambulia  njiwa weupe wawili waliorushwa na watoto waliokaribishwa na Papa Francis mapema siku ya Jumapili kwenye viwanja vya Mtakatifu Petro, uko Vatican.


Ndege hao waliwashambulia njiwa mara tu waliporushwa kutoka dirishani walipokuwa wamesimama watoto na Papa Francis

Inasemekana Njiwa hao walinusurika kwenye purukushani hiyo ya kushambuliwa na Kunguru pamoja na Shakwe na wakaweza kuruka na kupotea kusiko julikana. Ila hatima yao uko walipo haijulikani.

Njiwa wamekuwa wakitumika kama alama ya amani tangia enzi ya agano la kale. Na mwanzo wa kuwatumia njiwa kama alama ya amani ni pale Nabii Nuhu kwenye Biblia katika kitabu cha Mwanzo, alipomrusha njiwa ili kuangalia kama kuna sehemu iliyo kavu, na kwa bahati nzuri njiwa alirudi akiwa na jani la mzaituni kinywani. Ikimaanisha kuwa siku za mafuriko zipo ukingoni.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!