2 February 2014

Mwigizaji Maarufu Wa Holywood Philip Seymour Hoffman Afariki Dunia


Philip Seymour Hoffman (46), amekutwa amefariki dunia nyumbani mjini Manhattan.

Habari zilizotufikia kupitia vyanzo mbalimbali vya kuaminika ni kwamba, mwigizaji huyo alikutwa amefariki uku akiwa amejidunga sindano ya madawa ya kulevya mkononi mwake.

Kifo chake kinasadikiwa kuwa ni kutokana na matumizi ya kupitiliza ya madawa ya kulevya.
Marehemu aliwahi kushinda tuzo ya Oscar ya mwigizaji bora, alikutwa ameanguka na kufariki bafuni kwake, uku akiwa amevalia kaputula na fulana nyepesi na uku sindano ya dawa ya kulevya ikining’inia kwenye mkono wake.
 

 Marehemu amewacha kimada aliyekuwa akiishi naye kwa miaka isiyopungua 14 na kuzaa naye watoto watatu. Cooper mwenye umri wa miaka 10 na binti Tallulah miaka 7 na Willa mwenye umri wa miaka  5.


source: Dailymail
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!