17 December 2014

ALIYEKUWA mnenguaji mahiri wa bendi ya muziki wa dansi  nchini Aisha Mohammed Mbegu maarufu kama Aisha Madinda amefariki dunia  leo nyumbani kwao Kigamboni  Jijini Dar es Salaam

Kiongozi wa bendi ya Twanga Pepeta Luizer Mbutu amethibitisha kuwa Aisha amefariki dunia  na alifia nyumbani kwao sababu ambazo bado hazijafahamika.

Akizunumza kwa masikitiko Mbutu alisema kwamba  mwili wa merehemu umehifadhiwa katika Hospitali ya Mwananyamala.

Hapa nilipo natetemeka kwa msiba huu sababu marehemu alikuwa mzima na leo ndiyo ilikuwa aanze mazoezi na bendi ya Twanga Pepeta kwa ajili ya maandalizi ya onyesho la maadhimisho ya miaka 16 ya Luizer Mbutu ndani ya Twanga Pepeta alisema Luizer.

Aliongeza kwa kusema: "Hapa natetemeka  siamini lakini mwili nimeuona ni kweli Aisha amefariki na amefikishwa hapa hospitalini akiwa tayari amefariki.

Naye Mkurugenzi  Mtendaji wa  bendi ya Twanga Pepeta Asha Baraka pia amethibitisha habari hizo na hivi sasa yuko njiani kurejea Dar es salaam kwa ndege akitokea Kigoma ambako alikwenda kwa shughuli za uchaguzi wa serikali za mitaa.

Msiba uko Kigamboni  maeneo ya Mikadi Beach.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!