11 April 2013


Dalili na Viashiria vya ugonjwa wa kaswende

Dalili na viashiria vya ugonjwa wa kaswende hutegemea na aina ya ugonjwa wa kaswende wenyewe. Kuna aina tano za ugonjwa wa kaswende ambazo ni;

•Ugonjwa wa kaswende wa awali (Primary syphilis)
•Ugonjwa wa kaswende wa pili (Secondary syphillis)
•Kaswende iliyojificha (Latent syphilis)
•Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)
•Kaswende ya kurithi (Congenital syphilis

Kaswende ya baadae (Tertiary syphilis)

Asilimia 30 ya wagonjwa wa kaswende ambao hawakupata tiba hapo awali huingia kwenye kundi hili na hutokea miaka 15 – 30 baada ya maambukizi ya kaswende hapo awali. Aina hii inaweza kuathiri viungo kama macho, ubongo, mishipa ya fahamu (Neurosyphilis), jointi au viunganishi vya mifupa, uti wa mgongo, moyo, mishipa ya damu na hivyo kusababisha madhara makubwa kama;

•Upofu
•Magonjwa ya moyo – Aortic dissection type B, syphilitic aortitis
•Magonjwa ya akili
•Magonjwa ya mishipa ya fahamu
•Mtu kuwa kiziwi
•Kupungukiwa na kumbukumbu
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!