22 August 2014

Nimeipata hii sehemu kwa kweli nimeipenda Kama na wewe utapenda chukua huu ushauri.
Binafsi nilisha anza kuwaweka pembeni hao watu basic people ha ha ha ha

Hivi ndivyo alivyoanza....

Kuna baadhi ya LEVEL huwezi kufika...Kuna MAFANIKIO huwezi kuyafikia...Kuna HELA huwezi kuzipata...Kama umezungukwa na watu BASIC...
Kuanzia asubuhi mpaka jioni wanaongelea WATU TU..Fulani kamegwa na yule..halafu yule naniliu sasa hivi anatembea na yule ex wa nanii...Asubuhi mpaka jioni DISCUSSING PEOPLE...

Hawa ndio watu BASIC...Hata siku moja hawatakupa Ushauri kuhusu HOW TO REACH SOMEWHERE...NEVER
Na ukionekana unaanza kufanya vitu EPIC watakugeuka kwamba UNARINGA..UNAJISIKIA..UMEWATENGA...UNAJIDAI UNA HELA...and lots of bullshit...

Pengine ulipaswa kuwa mbaaalii kibiashara lakini HUWEZI sababu umezungukwa n Mbaazi tupu...BASIC PEOPLE...Ukiwaambia umesikia Kiwanja kinauzwa Kigamboni wanakwambia Kigamboni watu wanatapeliwa kuna mradi wa Joji Bushi...Ukiwambia unataka kujiunga Forever Living wanakwambia UNALIWA HELA...Ukiwaambia kuna SACCOSS wanatoa mikopo unataka uchukue ujenge wanakwambia INTEREST ZAKE UTASHINDWA na kujenga sio mchezo shosti..Unaamini unaacha!...Nataka kufanya Kitu flani WANAKUKATISHA TAMAA

Unahitaji kuzungukwa na watu wenye POSITIVE ENERGY ambao ukiwambia unataka kwenda Mbinguni kwa kupitia Mkuranga wanakuchangia Nauli...Niliposema naacha kazi watu ohh utakula nini..utaishije...Mji Mgumu huu..Wenzio wanatafuta kazi we unaacha utalosti...

WHO SAID??Nadunda kama kawa..Subaru inatembea kama kawa na Business zinaenda kama kawa...NEGATIVE PEOPLE WILL BRING U DOWN....Ukitaka Kupaa kaa karibu na ndege...We unataka kupaa unakuwa rafiki wa Nyangumi...UNAZAMISHWA SASA HIVI!!

Tangu nianze kukaa na watu Positive I have changed a lot...Nikiwaza jambo wanauliza HOW DO WE ACHIEVE THIS na sio FULANI ALIWAHIFANYA HII AKAFELI..
Ikikusaidia Chukua..
KILL ALL NEGATIVE PEOPLE AROUND YOU kama unataka kufikia Malengo Makubwa, I will be ur Lawyer at the Court na mwambie Hakimu nilikutuma mimi!

Akamaliza.

21 August 2014


Assalamu Alaiykum

Kuna siku moja nilikuwa naangalia kipindi katika Luninga (TV), walikuwa wakionyesha maisha ya wadudu mbalimbali. Mojawapo ya wadudu niliovutiwa nao ni Nyuki na wadudu wengine wa jamii ya Chungu (Ants).

Kwa kweli nilivutiwa sana na maisha ya hawa viumbe wadogo ambao katika maisha yetu hatuwapi nafasi hata ya kuwatafakari japo kwa sekunde chache tu. Ni mpaka pale tunapowaona kuwa ni kero ndio tunashtuka kuwa wapo.

Wadudu awa kwa kweli naweza kusema kuwa ni wadudu wenye uwezo mkubwa katika kukabiliana na maisha yao ya kila siku. Jambo moja niliovutiwa nalo ni jinsi ya mpangilio wa maisha yao katika mashimo yao na vichuguu vyao.

Kwanza kila mkazi wake anafata amri bila ya kusita. Jambo ili linastaajabisha kidogo, naanza ujiuliza nini siri yake. Muda nagundua kuwa, vichuguu hivi vya mchwa na hata makazi ya nyuki vimejengwa katika hali ambayo inampa nafasi kila mkazi, kufanya kazi zake bila tatizo lolote na bila usumbufu wa hali yoyote.

Kamera ya mchukuwaji wa hii picha naye anastahili sifa na ujasiri na uvumilivu kwa kweli, mchukuwaji wa picha ametuonyesha vyumba mbalimbali kwa kazi tofauti tofauti mfano, Maghala ya chakula ni makubwa na kila mchwa inakuwa ni rahisi kwake kufika hapo bila ya usumbufu wowote. Kuna vyumba kwa ajili ya kutotolea mchwa wapya na kuna sehemu maalum kwa ajili ya mawindo mapya na kile ambacho hakina faida au hawakiitaji basi wanakitoa nje kabisa ya kichuguu chao na kukitupa mbali.

Kwa kweli mambo nilio ona ni mengi lakini lengo langu si kuzungumzia maisha ya wadudu awa, japokuwa kuna mengi ya kujfunza kutoka kwao. lengo langu haswa ni kuangalia maisha yetu majumbani mwetu na jnsi tunavyoishi na kukusanya kila chenye uwezekano wa kukusanywa na kuwekwa kwenye majumba yetu.

Hebu angalia kwenye majumba yetu tunamoishi, na jinsi upangaji wa vitu mbalimbali ndani ya nyumba, yaani tuna shindwa na hata na wadudu katika mipangilio. Utakuta mtu kanunua fenicha mpya, lakini zile za zamani ambazo ukizionea aibu na ukutaka hata kuwakaribisha rafiki zako kuja nyumbani kwako, bado unazitafutia nafasi humo humo ndani. Kuzitupa au kuzigawa unaona tabu au siju unaona hasara, hakuna anayejuwa kwa kweli.

Utakuta nguo ambazo hazikutoshi tena, kuna zingine ulipewa zawadi ulipomaliza kidato cha nne ili ukatokezee kwenye mahafari ya shule miaka kumi kama si ishirini iliyopita, bado unazo, nguo haikutoshi tena, maana ushaongezeka toka kiuno nchi 28 mpaka sasa unavaa kiuno nchi 42, bado unayo tu, ukiulizwa eti kumbukumbu kutoka kwa mjomba wako.

Ukiingia uko kunakoitwa stoo, ni mazalia ya panya, mende na wadudu wengine wanaoishi bila ya kulipa kodi ya nyumba. Magodoro tangia ukisoma boarding school, na lile uliloanzia maisha ulipomaliza JKT ukahama nalo, bado unalo tu, japokuwa sasa ni mtu na familia yako na umekwisha nunua magodoro mapya, lakini yale ya zamani zamani badala ya kugawa umeviringisha na kuaweka juu ya kabati, maana kule stoo hakuna nafasi tena. Ukiulizwa unakiri kuwa kweli uvitumii kwa sasa, ila kuna uwezekano siku ukavitumia, lini haijulikani.

Uko kabatini kwako kuna nguo ambazo ulivaa ukiwa secondary mpaka leo bado unazo, ukiulizwa eti ni ukumbusho au utazivaa ukipungua, sasa utapungua lini, ulikuwa ukivaa kiuno 28 mpaka leo una kiuno 42 plus...

Uko jikoni ndio shida iliposhika hatamu! Mivyombo ya plastiki imepaukiana imeyayuka na moto ipo tu eti vyombo vya watoto, maana ukiwanunulia vya udongo awachelewi kuvunja, watakutia hasara.

Hotpot zote zimekata roho maana plastiki za nje zimepeana taraka na sufuria lake la ndani, lakini bado unalo tu. Kila ukibahatika kununu chupa za maji basi utahakikisha chupa zake huzitupi, vidoo vya sadolini, kila mahala hata hazitumiki zipozipo tu, hata maua hazifai kupandia we unazogo tu hutupi, na kuzihitaji wala huzihitaji.

Ukiangalia vyombo vya udongo vina mapengo na magego kama barabara iliyopigwa mabomu, na kila kimoja na dizaini yake havifanani kwa sababu seti zote zimesha vunjika vunjika hivyo ndio vimebakia.

Ukija ndani kwenye hiyo meza ya kuipambia, wenyewe mnaita Dressing table, ni hatari kwa kweli, maana imejaa mikopo na mibox haina hata kazi, perfume ya mwaka 2000 imekwisha malizika, weew kopo/chupa yake unayo tu, ukiuliza eti ukumbusho wa zawadi, ulipewa na nanii wako.

Uko stoo ukiambiwa uingie mwenyewe unaogopa, sababu stoo imekuwa mji wa panya na jamaa zao mende, maana imejaa vitu visivyo hitajika, stoo imekuwa ghetto la panya, maana vilivyokuwemo humo ni vile ambavyo huvihitaji tena, lakini kuvigawa au kuvitupa unaona hasara.

Sasa na lile pale nje nini niin, unaambiwa lile ni gari, unajuliza sasa mbona limebakia sikrepa tu, si uwape wanao kusanya vyuma, wakavipeleke kwa resaiko. Hutaki kisa ni gari la urithi la kutoka kwa baba yake na babu yako. Lipo tu hapo limekuwa makazi ya paka shume na wadudu wengine.

Kutupa vitu visivyo hitajika hamtupi eti Dhambi na kuvigawa haviwezekani tena maana havina hadhi tena ya kupewa mtu, vimekosa ile uhalisi wake, hakuna hanaye vitaka wala kuviulizia.

Ndio maana kila siku hamuishi kupishana mahospiitalini, mara leo kikohozi kesho kifua kizito, mara mafua na flu. Kwanini msiumwe na mnakaa dampo!?

Tumewaambukiza mpaka watoto wadogo, maana wanajuwa kuwa nyumbani kwao hata kikopo cha icecream au kopo la plasitiki la siagi havitupwi vinaoshwa vinawekwa hapo. Halafu bado unaendelea kumuomba Mungu akupe, akupe uweke wapi na kwako pameshajaa au uoni!?

Huu ni ugonjwa? Na wengi tumehathirika na haya maradhi ya kutopenda kutupa au kugawa tusivyo vitumia wenye lugha yao wanaita "hoarder disorder".

20 August 2014


Mwanamume mmoja mkazi wa Saudia, ametoa kali ya mwaka pale alipotimua mbio kiasi cha kuwashangaza watu wa usalama wa kiwanja cha ndege katika moja viwanja vya ndege nchini Saudia.

Mwanamume huyo mwenye asili ya Misri alikubali kumuoa mwanamke kutoka nchini kwao Misri, baada ya kuonyeshwa picha yake na kaka yake.

Bwana harusi aliwasili kiwanja cha ndege mapema uku akiwa na hamu na bashasha tele na tabasamu kubwa akimsubiri bibi harusi kwa saa kadhaa, kabla ya ndege iliyomleta bibi harusi kuwasili kiwanjani.

Mwandishi wa Gazeti la Kiarabu la nchini Misri Al Watan litokalo kila siku, amenukiliwa akiripoti kuwa...
"Baada ya bwana harusi kutambulishwa na kumuona bibi harusi, ghafla alitimua mbio kama mtu aliyeona mzuka au kitu cha kutisha.

Kiasi cha kuwafanya walinzi na watu wa usalama wa kiwanja cha ndege kumkimbiza wakidhania kuwa ameiba kitu."

Gazeti ili limenukuliwa bila kutaja majina ya wahusika wala kiwanja cha ndege, lilipotokea ilo tukio.

Baada ya wana usalama wa kiwanja cha ndege kumkamata bwana harusi, walimuhoji kilichomfanya mpaka kutimua mbio kiasi kile, naye alinukuliwa akisema kuwa. "Alishtushwa na mwonekano wa bi harusi na hataki tena kuwa pamoja naye wala kuishi naye kama mume na mke."

Bibi Harusi aliomba talaka kisheria pamoja na fidia kwa kupotezewa muda wake.

18 August 2014Anaitwa Sewa Haji Paroo alifika Zanzibar akitokea katika wilaya Kutch katika jimbo la Gujarat, nchini India. Mnamo mwaka 1852 alifungua duka la bidhaa mbalimbali huko Zanzibar. Mnamo mwaka 1860 akafungua duka lingine kubwa mjini Bagamoyo na kuweka makazi yake uko.

Biashara zake zikawa kubwa na kuwa tajiri mkubwa sana, alisaidia watu wote bila kujali rangi, dini wala kabila zao. Alinunua majengo mengi na kuyafanya maeneo ya watu wasiojiweza, alijengaja mashule na hospitali kadhaa, katika mji wa mzizima (leo inaitwa Dar ES Salaam). Alijenga hospitali na Kuiita Sewa Haji, ikitoa huduma bure.

Mnamo february 1897 Sheikh Sewa Haji Paroo alifariki dunia, ilikuwa ni huzuni na simanzi kwa wakazi wa Bagamoyo na Mzizima kwa kuondokewa na Sheikh Sewa Haji, maana aliependwa sana na wananchi.

Baada ya kifo chake wakoloni baadaye wakabadilisha jina kutoka Sewa Haji Hospital na kuiita Princess Magreth Hospital, na mnamo 1963 iliitwa ikabadilishwa tena jina na kuitwa Muhimbili Hospital, na wakaipa mojawapo za wodi jina lake Wodi ya Sewa Haji.

MwenyeziMungu Amlipe kila la Kheri Shekhe Sewa Haji, kwa kila jambo la kheri alilolifanya na amsamehe makosa yake.
Aamiyn

14 August 2014

Shule ya Msingi, iliyoko kwenye majengo ya Msikiti wa Mtambani wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam umeteketea kwa moto.

Taarifa zilizopatikana kutoka kwa mashuhuda wa tukio hilo wamesema kuwa, shule hio imeteketea kwa moto jana jioni na hakuna aliyejuruhiwa katika tukio hilo.

Walioshuhudia tukio hilo walisema kwamba moto huo ulizuka ghafla baada ya Swala ya Magharibi na kuteketeza sehemu yote ya juu ya msikiti huo, ambako ndiko kwenye majengo ya shule ya msingi.

 
12 August 2014


Mwigizaji na mchekeshaji maarufu na mshindi wa nishani ya mwigizaji bora (Oscar-winning actor), amefariki dunia siku ya Jumatatu, 11th Agosti 2014. Habari zilizoko kwenye vyombo vya habari ni kwamba, Robin Williams amejiiua akiwa nyumbani kwake uko Kaskazini mwa California akiwa na umri wa miaka 63. Msemaje wake Buxbaum aliwaambia waandishi wa habari katika taarifa kuwa... Hivi karibuni Williams alikuwa anaosumbuliwa na unyogovu wa akili (depression), tatizo ambalo limesababishwa na matatizo ya unywaji mkubwa wa pombe. Ni tatizo ambalo limekuwa likimsumbuwa muda mrefu wa maisha yake.

Baadhi ya filamu alizo igiza ni kama hizi:

The World According to Garp (1982), Good Morning, Vietnam (1987), Dead Poets Society (1989), Awakenings (1990), The Fisher King (1991), and Good Will Hunting (1997), Popeye (1980), Hook (1991), Aladdin (1992), Mrs. Doubtfire (1993), Jumanji (1995), The Birdcage (1996), Night at the Museum (2006), and Happy Feet (2006), Everyone's Hero (2006), RV (2006), The Night Listener (2006), License to Wed (2007), August Rush (2007), Shrink (2009), World's Greatest Dad (2009), Night at the Museum: Battle of the Smithsonian (2009), Old Dogs (2009), Happy Feet Two (2011), Stage Left: A Story of Theater in the Bay Area (2011), The Big Wedding (2013), The Face of Love (2013), The Butler (2013), Boulevard (2014), The Angriest Man in Brooklyn (2014), Merry Friggin' Christmas (2014), Night at the Museum: Secret of the Tomb (2014).

10 August 2014

Mie ni mpenzi mzuri wa movie za kizungu  na kihindi na pia huwa nafuatilia Sana maisha yao. 
Naomba sana siku moja hii iwe inawatokea WASANII wa nyumbani.

Hiki ndio alichoandika mr mwenyewe
Na hii ni picha yake au post yake ya 674 ktk mtandao wa face book

FB 674-Sunday well wishers back again even after 32 years they still come...!!so humbled and filled with gratitude! Iwas away for a few Sundays but they still come so this evening it was a reunion...

Amitabh BachchanMashabiki wakiwa nje ya nyumba ya mr Bachchan 
Yaani hawa wanaenda pale kumuona tu

9 August 2014

 
Katika pitapita zangu Mitandaoni, nikiokoteza iki na kile, ghafla nikakutana na simulizi iliyovuta macho yangu, kiasi nikaona si vibaya nikaisoma na kushea na wadau, labda nao wanaweza kufaidika kwa namna moja au nyingine. Kumbuka kuwa haya ni mawazo yake mwandishi na hayana uhusiano wowote na blog ya Tmark-Turn. Kichwa cha bandiko ili kilikuwa:
Ndugu zangu sio kila kinachonga'aa ni dhahabu majuu sio mchezo, Nimekibadilisha na kuipa jina lingine Maisha Ughaibuni, ili kuvutia wasomaji wetu.

- Leo naomba mnipe nafasi nijaribu kuwasaidia baadhi ya ndugu zangu Wabongo ambao hawajafika Majuu na wanaota kufika huko, kwenda kutafuta maisha maana wanaamini kule ni Paradise.

Binafsi nilikuwa na hiyo ndoto nikaitimiza na kujionea mwenyewe na nikajifunza kwamba sio kila kinachong'aa ni dhahabu. I was once a believer of that theory kwamba Majuu ndio kila kitu mpaka nilipofika huko na kujionea mwenyewe kwa macho yangu baada ya kuishi huko miaka 30.

- Kwanza ukifika tu kama nilivyokwenda New York City/USA wabongo wenzako hata unaowajua wanakukimbia maana hawawezi kukusaidia, tatizo la kwanza makaratasi ya kukuwezesha kufanya kazi tena kazi ambazo kwenye maisha yako hapa bongo hukutegemea kuzifanya infact ni kwa mara ya kwanza nikaona Singa singa anafanya kazi kituo cha mafuta sikutegmea kuona hayo hata siku moja.

Huna makaratasi na huna pa kukaa kama umeenda kama nilivyokwenda mwenyewe kivyako vyako, itakuchukua miezi kama 6 ya kusota sana ndio uweze kupata ID na Card ili uweze kupata kazi angalau ya kulea wazee au matahira.

- So kwa mara ya kwanza katika maisha yako unakutana na kitu kinaitwa Kodi, au taxes maana hapa bongo tunacheza cheza tu na kodi kule ni serious ishu, panga pangua huwezi kupata mshahara unaozidi Dola 500 za kimarekani kwa wiki kati ya hizo watakukata angalau 100 za kodi so utabaki na 400 tu chumba 150 kwa wiki, nauli ka kwenda na kurudi kazini, halafu unagundua ili upate hgela extra ni lazima ufanye kazi masaaa mengi, so kwa mara ya kwanza unajifunza kuishi kazini maisha yako yanakuwa ni kazini tu,

- Wazungu wana akili sana System yao wameitengeza makusudi kwamba mtu kama wewe mbongo ukienda unaichangia Uchumi wao tu, uwezekano wa wewe kuwa tajiri kwa kufanya biashara kule haupo kabisa unless uuze madawa ya kulevya, ninasema tena uwezekano wa wewe mbongo kutajirika

Majuu ni haupo kabisa labda ujiunge na kuuza madawa ambayo haitachukua muda mrefu watakushika unajua kwa nini watakushika ni kwa sababu Polisi wa majuu wana akili sana wanajua kwamba hawawezi kuzuia kabisa kuuzwa madawa ya kulevya kwa sababu moja kubwa sana nayo ni Law Enforcement ya kuzuia drugs inaajiri karibu wananchi Millioni 2 wa taifa lao.

Sasa ukizuia madawa ina maana hawa hawatakuwa na kazi kwa hiyo wanavyojifanya wanazuia madawa ni waongo sana nalijua hili kutokana na kusoma Criminology nchini kwao, so wanachofanya ni kwamba kwa mfano Mjini New York.

Polisi wameugawa mji mzima kwa vipande vipande na kukata maeneo ya wauza drugs, wanaowajua one on one lakini hawawashiki hata siku kwa sharti moja tu kwamba wasiue au wasuze ile drugs ya kujipiga sindano, kwa hiyo any crime ikitokea kwenye lile eneo polisi wanamfuata muuza drugs mkubwa pale waliomkabidhi eneo ambaye siku zote ana wafanyakazi wengi mtaani kwa hiyo anajua nani amefanya anawaambia.

Polisi mara moja unashikwa, sasa wewe mbongo kwa vile hujui hii system unajiingaiza na kuanza kuuza drugs, mwenye eneo anakujua mara moja na kuwashitua Polisi ndio mwisho wako na Polisi wa Majuu hawana haraka wanaweza kukuwinda hata mwaka mzima nia na madhumuni yao kukamata system yako nzima na watakushika tu.

- Biashara ya halali huwezi kwa sababu kwanza huna capital ya kutosha na besides Wazungu wameshazoeshwa majina makubwa so siku zote wananunua kwenye maduka yenye majina makubwa, pili kodi ni kali sana huwezi kabisa maana kwenye kulipia kodi utashindwa tu so wabongo wengi majuu wanaojifanya kufanya biashara ninasema ni waongo sana always wana biashara nyingine kuliko wanayoionyesha.

- So huna choice ila kufanya kazi tu kama mbwa, ukitoka kazini ni kulala tu na kukaa ndani ya nyumba kuangalia TV hela huna mpaka mwisho wa wiki ukilipwa Wazungu wajanja sana wanakulipa kila mwisho wiki kusudi uweze kuzitumia hela zote by jumatatu ndivyo uchumi wao unavyosimama imara.

Wazungu wanajua kuwa hela wanazokulipa mshahara hazitoshi kwa hiyo wamekutengenezea system ya Credit Card yaani unapewa Card bila masharti magumu ukope, kufumba na kufumbua una madeni kuliko uwezo wako, hatimaye wanakufikisha mahali unakuwa unalipa madeni yako on interest tu bila kugusa deni lenyewe hasa deni linaendelea kuwa kubwa mpaka mwisho maisha yako ni madeni tu,

- Huku home ndugu na jamaa wanakuaminia kwamba sasa upo vizuri kumbe sio kabisa, kutuma hela huwezi wewe mwenyewe huna hela extra maana ile system haikupi hiyo nafasi, so Rafiki yako wa bongo akija unamkimbia maana huna hela extra ya kumsaidia unajificha mpaka usikie amekuwa sawa ndio unajitokeza na kujifanya kumjua sana na kwamba ulikuwa umesafiri, ndugu yako akija unamkimbia maana huwezi kumsaidia hatimaye unakata mawasiliano na home bongo maana huna pesa.

Pole pole unaanza kuwa kama Wazungu ukitembea unaongea mwenyewe kudadeki madeni yamekukaba mpaka shingoni, zamani ilikuwa rahisi ukizidiwa madeni unaenda Mahakamani una-file kufilisika wanakusamehe siku hizi hamna tena hiyo mpaka ulipe tu.

- Sasa unaanza kukumbuka bongo, hapa ulikuwa na kazi nzuri ulikuwa unaweza kula mara tatu kwa siku unaweza kwenda bar kunywa kidogo, unaweza kwenda uwanja wa Taifa kuona mipira mikubwa.

Majuu forget it it will never happen huwezi so huna pa kwenda matokeo yake mbongo mmoja akifanya party ya birthday hata ya mtoto mchanga wote mnakimbilia huko watuwazima unakuta mmejaa nyumbani kwa mbongo, kijumba kidogo mnabanana humo humo na kuanza kupiga picha za kutuma bongo kuwakoga wajinga kwamba upo majuu.

Pale kwenye party inatakiwa uwe very careful kwenye kupiga picha unatafuta angle ya kuonyesha upo kwenye bonge la nyumba kumbe mazishi matupu, umevaa nguo za kukopa dukani kwa credit card, kesho kazini mapema sana so hata pale kwenye party huna raha ila unajifanya kuwa furaha sana kumbe uongo mtupu madeni yamekukaba mpaka shingoni masikini wa Mungu,

- Matokeo yake unaanza kuja kwenye mitandao na kuanza kutukana Serikali ya Tanzania na Viongozi wake kisa na mkasa yamekushinda huko Majuu, na kurudi huwezi wengi wao wanaanza ku-develop tabia za ajabu na kutisha sana kisa maisha ni magumu na sivyo walivyotegemea lakini hawawezi kukubali na kusema wazi maana ni aibu.

Wazungu wametengeneza system yao ya maisha ili wanasheria na madakitari tu ndio wale bataz so wewe ukienda kule bila kusoma utachekesha tu, na uzuri wa Wazungu ni kwamba no matter what utakula tu maana kwa mfano usiku fast food zote wanatakiwa ikifika saa sita kutupa chakula kama kipo hakiruhusiwi kwenda next day kwa hiyo ukienda pale watakupa bure maana hawaruhusiwi kukitupa mpaka wahakikishe hakuna mtu anayekihitaji kwanza ni sheriaa.

- So unaanza pole pole kukumbuka bongo, furaha yako yote haipo tena Wazungu kama kawaida yao hawapendi weusi popote unapokwenda wewe ni nothing but nigga, huna thamani yoyote ni good for nothing halafu maisha majuu ni sheria asubuhi mpaka saa ya kulala!!!.........

OK GUYS KWA LEO NAOMBA NIISHIE HAPA NEXT NIKIWA NA TIME KAMA YA LEO WILL DO SOME MORE!!

Le Mutuz

6 August 2014

Magadi Soda:

Magadi soda ni mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Changanya kiasi kidogo cha magadi soda na maji ya kutosha kuunda kidonge kidogo na kisha weka au kandika kidonge icho sehemu ilio athirika na chunusi. Kwa muda wa dakika 15-20 au mpaka ikauke, na kisha suuza kwa maji yasiwe ya moto. Unaweza kurudia rudia mara kadhaa kwa siku mpaka utakapo ona athari ya chunusi imepotea.

Matango:

Unaweza kutumia Tango kwa kuondoa chunusi na hata kuondoa mabaka mabaka katika ngozi na kuifanya ngozi yako kuonekana yenye afya na yenye kuvutia.
mazuri sana kwa kusafishia uso na haswa ukiwa na chunusi. Kata tango na kasha liponde ponde (unaweza kutumia blenda) kisha paka au kandika usoni. Wacha ikae kwa muda wa dakika 15-20  kisha suuza kwa maji baridi. Unaweza kurudia kwa siku mara mbili mpaka mara tatu kwa siku.

Kitunguu Thaumu:

Unaweza kutumia kitunguu thaumu. Kuondoa chunusi. Matumizi ya Kitunguu thaumu, uleta matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na hata kuuwa bacteria sababu ina kemikali (antiseptiki) inayozuia kukua kwa bakteria kwenye jeraha au ngozi iliyo athirika kwa chunusi au hata kwenye kidonda. Na pia ina viwango vya juu wa salfa (ni zuri kwa ajili kukausha mafuta kwenye ngozi ya mwili). Twanga kitungu thaumu, au unaweza kukata nusu na kubandika sehemu iliyo na chunusi shikilia kwa dakika 5-10, na kisha safisha na maji baridi. Waweza kufanya ivyo asubuhi na jioni.

Mnana (Peppermint):

Unaweza kutumia majani ya Mnanaa kuondoa chunusi usoni.
Majani ya manna utumika hata kwa wale wenye matatizo ya Mba kwenye kichwa. Twanga majani machache au saga kisha weka sehemu iliyo athirika. Wacha mpaka pakauke na kisha safisha kwa maji baridi. Unaweza kufanya hivyo mara kadhaa kwa siku.

Matumizi ya Limao:

Kata limao na kisha kwa kutumia kijiti chenye pamba kiloweke kwa maji ya limao, sugua sehemu yenye chunusi, kisha wacha pakauke, unaweza kurudia rudi kila baada ya masaa kadhaa. Usitumie maji ya limao ya kwenye chupa, kwa sababu yameweka vihifadhi kemikali zingine kiasi cha kuondoa ubora wa kemikali halisi za kwenye limao. Tumia limao alisi.

Kutumia Asali:

Matumizi ya asali ni ya asili na ufanya ngozi, iwe na afya na nyororo. Kwa sababu kwenye asali kuna virutubisho vingi vyenye kazi ya kuua vimelea (bacteria) na kuzuia uchafu na kusinyaa kwa ngozi.
Weka asali kidogo sehemu ilio athirika na iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Vilevile unaweza kupaka uso mzima au hata mwili mzima ukitaka. Sababu asali inarutubisha ngozi ya mwili na kuifanya iwe na afya na mwonekano mzuri. Ukisha ridhika na muda wa asali kwenye ngozi yako unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya vuguvugu.

Kutumia Papai:

Unaweza kushangaa, lakini matumizi ya papai yameonyesha matokeo mazuri sana katika kuondoa chunusi usoni na kusafisha sehemu zingine za mwili.
Ponda ponda kiasi kidogo cha papai na kisha iwache kwa muda mrefu kadri uwezavyo. Ukisha ridhika na muda unaweza kusafisha kwa kutumia maji ya kawaida. Unaweza kurudia mara kadhaa kila siku kama unataka.

Dawa Ya Meno:

Unaweza kushangaa, lakini ushangazwi na matokeo mazuri ya meno yako kusafishika kwa dawa ya meno.
Kemikali zinazotumika kuuwa Bakteria wa kwenye meno, pia zina uwezo wa kupambana na bakteria wengine. Tumia dawa ya meno isiyo na gel (non-gel) paka kwenye chunusi. Ni vizuri ukatumia usiku wakati wa kwenda kulala, ila si vibaya ukipaka hata muda wa asubuhi au mchana mradi tu uwe na muda wa kutosha wa dawa kukauka ili iweze kufanyakazi vizuri.

Namna nyingine ni kuchanganya dawa ya meno na unga wa mahindi au nganoiuliosagwa na kuwa laini sana. Unaweza kupaka na kuiwacha ikauke kwa dakika tano mpaka 10.
Safisha kwa sabuni. Mchanganyiko huu unasaidia kukausha chunusi.

Matumizi ya Poda:

Unaweza kutumia baby powder kwa kupaka nyakati za usiku wakati wa kwenda kulala na na kuiwacha mpaka asubuhi.

Matumizi ya Mvuke:

Unaweza kutumia mvuke (Steam/vapour) kuondoa mafuta yaliozidi kwenye ngozi ya uso wako. Kwa kujifukisha. Kwa wale ambao hawana mashine wanaweza kujaza sufuria au bakuli kwa maji ya moto na kujifunika kwa taulo uku ukielekeza uso wao kwenye sufuria au bakuli lenye maji yanayotoa mvuke k wa dakika 5-10. Unaweza kufanya hivi pamoja na njia mojawapo nilizo zitaja hapo juu.

Tahadhari:

Njia hizi za Asili, uchukuwa muda kidogo mpaka kuona matoke ya kuridhisha.
Njia zote hizi kama hazijaleta matokeo mazuri, tafadhali muone daktari wa ngozi au nenda hospitali ilio karibu kwa uchunguzi zaidi wa ngozi yako.
 
Sabuni pia zinasemekana kuwa na kemikali zinazoathiri mbegu za wanaume

Kemikali zinazopatikana katika baadhi ya bidhaa ambazo hutumiwa kila siku kama vile dawa ya kusugua meno, sabuni na mafuta ya kujikinga kutokana na miale hatari ya jua zinaweza kuharibu mbegu za uzazi za wanaume.

Kwa mara ya kwanza watafiti wanaonya kuwa bidhaa hizo zina uwezo wa kuanthiri uwezo wa mbegu za uzazi za wanaume kuzalisha mwanamke.

Wanasayansi hao wanasema kwamba bidhaa hizo zina kemikali ambazo zinachangia matatizo ya uzazi kwa wanaume katika nchi za magharibi.

Kemikali zinazopatikana katika dawa za kusugua meno zinasemekana kuharibu nguvu za mbegu za kiume kuweza kuzalisha.

Takriban mwanamume mmoja kati ya sita aliyeoa nchini Uingereza anakumbwa na tatizo la kuzalisha na tatizo la utasa ndio kiini kikubwa cha hali hiyo.

Uchunguzi huu ulifanywa na watafiti kutoka Uingereza na Uholanzi na walifanyia uchunguzi kemikali 100 kila siku huku wakigundua kuwa thuluthi moja ya kemikali hizo ziliathiri uwezo wa Manii kufikia katika mayai ya mwanamke.

Utafiti huu uliandikwa katika jarida la afya la EMBO na watafiti wanasema nyingi ya kemikali hizo hatari zinapatikana katika mafuta yanayotumiwa kujizuia na miale hatari ya jua.
Kemikali nyingine inajulikana kama Triclosan, ambayo inapatikana katika sabuni na dawa ya kusugua meno.

Uchunguzi wa maabara ulionyesha kuwa kemikali hizo zinaathiri uwezo wa Manii ikitafuta mayai ya mwanamke kuweza kuizalisha.
Kadhalika kemikali hizo pia zinaharibu kabisa manii kiasi cha kukosa hisia kwa homoni za mwanamke.
 
Dawa ya meno inaweza kuathiri mbegu za uzazi.

Mabadiliko haya yanapotokea kwa mbegu za kiume, huifanya kuwa vigumu kuweza kuzalisha.
Watafiti hao wanasema kuwa mchanganyiko wa kemikali hizo ni hatari zaidi kwa mbegu hizo.

Kemikali hizi hujulikana kama kemikali zinazoathiri jinsia kwa sababu ni sehemu ya kemikali zinzzoathiri homoni za mwili wa mwanamume.
Mwaka jana shirika la afya duniani lilihusisha kemikali hizo na saratani ya matiti na pumu.


Inaelezwa kuwa benki ya mbegu za kiume itatatua haja za uzazi
Benki ya Taifa ya mbegu za kiume inatarajiwa kuanzishwa nchini Uingereza kuondokana na tatizo la upungufu wa mbegu hizo.

Wapenzi wa jinsia ya kiume na kike , wale wa jinsia moja pia wanawake wasio na wenza watanufaika na huduma hii mpya ambapo kutoka jamii zisizofahamika watakuwa na uwezo wa kuchagua wachangiaji kutoka katika jamii nyingine.

Benki hii itakayosimamiwa na Mfuko wa Taifa wa Gamete na Hospitali ya Wanawake ya Birmingham itafunguliwa mwezi Oktoba.

Mradi huu umetengewa paundi 77,000 na Idara ya Afya nchini Uingereza.
Kituo hiki kitakuwa katika hospitali ya wanawake mjini Birmingham ambacho kitakuwa kikihifadhi mbegu hizo.

Hivi sasa kumekuwa na upungufu wa wachangiaji wa mbegu za kiume nchini Uingereza hasa katika hospitali za taifa,huku kukiwa na ongezeko la uhitaji, hospitali hizo zikitibu tatizo hilo linaloelezwa kuwa kubwa nchini humo.

Mfuko huo umesema una matumaini kuwa uwepo wa benki hiyo utapunguza idadi ya wagonjwa wanaojiweka katika hatari kwa kutafuta huduma hii bila kufuata taratibu.

4 August 2014


Baby Fatma na dadake wakifurahia summer katika maadhimisho ya 6 ya Kila Mwaka ya kukimbiza vimipira (Annual Barrack Hill Ball Run) katika Mji wa Cobh. katika kusaidia Brainwave, Cancer Research.27 July 2014

Assalamu 'Alaykum wa RahmatuLlaah wa BarakaatuhJumatatu In-shaa-Allah ni tarehe 1 Shawwaal 1435H (28 July 2014) na ndio Siku kuu yetu ya ‘Iydul-Fitwr.

Kwa Munaasabah huu wa furaha ya siku hii tukufu ya ‘Iyd Al-Fitwr Napenda kuchukua fursa hii kuwawasilishia salaam zetu mimi na Familia yangu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu.

26 July 2014

Hatari hii yote kunatafutwa pipi jamani huyu Mtoto anataka kuniletea polisi nyumbani Kwangu na yeye ninyan'ganywe
Pipi tu hizo zinataka kuleta balaa
Piga kelele sana somebody help me nawe bingwa msaada wa nini?
Balbriggan Integration Forum (BIF) was nominated by Fingal County Council to take part in the Pride of Place competition. Pride of Place is an honorary recognition of a group, place or a community for the valuable work undertaken in their local areas. BIF is set to win this for Balbriggan. 
Okey mie ndugu yenu niliwakilsha Tanzania na nilipika vitumbua,na nikapata muda wa kuilezea Tanzania kwa kidogo.

   Mwenye nguo nyeusi na weupe ndio muandaaji wa hii siku anatokea serrileon 
Besty Abu

 Bazungu walivutiwa sana na vitumbua hahahaha ��


    Mwishoni hapo unaona bendera ya   Tanzania eeeh na bakuli la vitubua in baby T voice.
    Huu msosi toka Eltria 
 Wenye nchi Yao wa kwanza hapo Ireland
   Sahani mbili za kwanza toka Romania ,
Hizo zinazofuatia toka Rusia 
Na hilo sosi hapo toka Jamaica 
   Hapo bendera zinajieleza
   Eltria 

20 July 2014

Hivi kweli jamani hakuna kazi za kufanya mpaka kutapeli?

Hii nimeitoa katika USO wa kitabu(face book) rafiki yangu Belinda Ndio ametuma hii stori.

, kuna incident imetokea maeneo ya sinza naomba niwarushie kama ilivyo ili tujifunze kitu
: leo asubuhi wamekuja watu 6nyumbani wakasema wanatoka tanesco wamekuja kucheki mita ya luku.wakakorokocha wakasema mita imechezewa kwa hiyo wanakata umeme na kung'oa mita, eti waliona kwenye gps yao kuwa umeme hauendi vema.��yakatutoka,wakasema fidia na kurudisha umeme kiofisi ni milioni 8! ila tukiwapa milioni 2 wataturudishia.nikawauliza kama mita imechezewa mbona tunanunua umemewa laki 3 kwamwezi?si ingepaswa tulipe kidogo?wakasema wakati mwingine wakiweka hiyo resistance (eti ndo kifaa cha kuiba umeme) huwa kinafyatuka halaf umeme unakwenda zaidi! wakakata umeme wakaondoka,tujipange.tujadiliana na mzee tukapata mashaka maana walikuwa wakali halaf wanalazimisha mambo,wamevaa vitambulisho lakini wamevigeuza kwahiyo havisomeki.tukapiga simu tanesco kuwauliza wakasema hao ni vishoka tuite polisi.basi tukawapigia simu waje wachukue laki tano waturudishie umeme,mengine j3. wakaja fasta2 wakarudisha umeme.nikawaambia naenda atm wasubiri.nikawaacha na mzee.nikatoka mbio mpaka polisi chuo nikawahadithia wakanipa polisi 3 nikaja nao home,tukawakuta wameondoka.mzee akawapigia simu waje hela imepatikana.wakasema tukutane mlimani city,tukafanikiwa kukamata mmoja wengine wakakimbia.tumemuacha selo,tukaandikisha maelezo.tunasubiri hatua itakayofuata.hiyo picha ndo huyo tuliyemkamata!

16 July 2014

WASIOJUA kuhusu uwezo wa asali na mdalasini wanaweza wasiamini wakiambiwa kuwa vina uwezo wa kuzuia na kutibu magonjwa hatari yaliyoshindakana hata hospitalini. Asali na mdalasini zimekuwa zikitumika kama tiba tangu enzi na enzi.

FAIDA ZA ASALI NA MDALASINI KIAFYA
Asali na mdalasini bado inaendelea kutumika kama tiba katika magonjwa ya aina mbalimbali, hasa kwa baadhi ya watu wanaoamini katika tiba mbadala kuliko tiba za kisasa, na kwa kiwango kikubwa wameweza kutibu maradhi yao bila kupata athari zingine.

Kwa mujibu wa tafiti mbalimbali za kisayansi, asali ina dawa asilia ya kuua vijidudu mwilini (anti- bacterial properties). Kama ukiweka asali kwenye kidonda au mahali ulipoungua na moto, utazuia maambukizi na utaponya kidonda pia.

Ulaji wa mara kwa mara wa asali na mdalasini kwa pamoja, hutoa kinga dhidi ya ugonjwa wa moyo, kwani vyakula hivi husafisha mishipa ya damu na huyeyusha mgando wa damu kwenye mishipa. Kuziba kwa mishipa huwa ndiyo chanzo cha tatizo la shinikizo la damu na magonjwa ya moyo.

Unywaji wa asali iliyochanganywa na mdalasini kwenye maji ya uvuguvugu, utasaidia kusafisha kibofu cha mkojo na hivyo kuondoa maambukizi yoyote yanayoweza kuwepo kwenye kibofu. Kwa maana nyingine, kwa kupenda kunywa mchanganyiko huo, utajiepusha na matatizo ya kuziba kwa haja ndogo na hata saratani ya kibofu kwa kukiweka kibofu chako salama kila wakati.

Aidha, unywaji wa mara kwa mara wa mchanganyiko huo, hutoa nafuu kubwa ama huweza kuponya kabisa wenye matatizo ya ugonjwa wa baridi yabisi (arthritis). Mgonjwa anywapo mchanganyiko huu, maumivu hutoweka mara moja na kumpa nafuu ya haraka.

Vilevile, unywaji wa mchanganyiko wa asali na mdalasini huimarisha kinga ya mwili na huweza kuondoa magonjwa yote ya kuambukiza kama vile mafua au flu na huondoa mwilini baadhi ya vijidudu vinavyoambukiza magonjwa mbalimbali. Ukitengeneza mchanganyiko mzito wa asali na mdalasini na kupakaa kwenye jino linalouma utapata nafuu haraka na utazuia pia kuendelea kuuma kwa jino.

Asali na mdalasini ikitumiwa kwa pamoja pia, husadia usagaji wa chakula tumboni na hivyo kuwezesha upatikanaji wa choo laini na huzuia tumbo kujaa gesi. Asali na mdalasini pia huongeza nguvu mwilini na huchangamsha ubongo na kumfanya mtu kuwa mchangamfu kazini.

Kuna tafiti nyingine zinaonesha kuwa asali na mdalasini humuwezesha mtu kupunguza uzito kirahisi na ni kinga imara dhidi ya baadhi ya saratani. Hata hivyo, inashauriwa kutegemea vyakula hivi maarufu katika kutoa kinga ya maradhi kuliko kutegemea kama tiba zaidi, kwani kwa baadhi ya magonjwa sugu haviwezi kuponya kwa haraka.

Ili kupata faida ya asali na mdalasini kama kinga, ni vizuri kuzingatia kanuni za ulaji sahihi kwa ujumla na kutumia vyakula hivi kama sehemu ya mlo wako wa kila siku sambamba na vyakula vingine sahihi, huku ukizingatia suala la kuushughulisha mwili kwa mazoezi na kazi.

Leo nilikuwa nimekaa peke yangu barazani, nikitafakari hali ya maisha kiujumla, mawazo yakanichukuwa na kunipeleka mbali kiasi, yaani miaka michacahe iliyopita, si miaka mingi sana ni kiasi cha miaka thelathini mpaka arubaini iliyopita, enzi zile kabla hizi simu za mkononi hazijaingia uku kwetu Bongoland.

Enzi zile kutembeleana ilikuwa ni jambo la kawaida sana na tena wakati mwingine bila hata ya taarifa, waweza kumshtukia aidha rafikio au nduguyo toka mkoani amekuja na mabegi na vikapu vyake vya vyakula, kaja kukujulia hali.

Hali hii ilikuwa ni kawaida sana na kama imetokea ujaonana na rafikio au nduguyo kama si jamaa yako basi aidha utamwandikia barua ambayo inaweza kuchukuwa wiki kama si mwezi kufika uko ulikoituma na ikitokea mmeonana mtaani basi ni lawama za hapa na pale, kosa ni kutotembeleana.

Hali hii siku hizi imeondoaka nikawa najiuliza, kulikoni mambo haya, kumepita maswahibu gani hapa, siku hizi kutembeleana imekuwa mpaka msiba au harusi ndio utawaona ndugu na jamaa wakipiga hodi nyumbani kwako. Baada ya kutafakari kwa kina nikagundua kuwa haya maendeleo ya simu na mitandao ndio imepelekea mpaka ndugu na jamaa kutotembeleana tena.

Maana ukitaka tu kujuwa hali ya nduguyo au jamaa yako basi vidole vinafanyakazi, na teba siku hizi simu za smatifone ndio kabisa, maana hata ukitaka kumuona nduguyo wee unabofya tu, mara whatsapp, viber au skype, mwaonana hivi na kuzungumza. Hali hii kwa kiasi Fulani nahisi kama imeondoa uhalisia wa binadamu kutembeleana na hata mapenzi kidogo yamepungua, maana kama mtu una hamu ya nduguyo au jamaa yako, huna haja tena ya kufunga safari na kwenda kumsalimia, we wabofya tu, bofyoo, mnayamaliza kwenye simu.

Tena hizi simu za kisasa ukifanya mchezo kwa wale walioko kwenye ndoa unaweza kugombana na mwenziwako, maana hakuna tena yale mahaba mkikaa mmekaribiana, maana kila mtu yupo bize akibofya na kubofyoa, mara wasapu mara vaiba, mara skaipu, akichukuwa umbea wa uku akipeleka uku, wa kule akipelekea kule, bize kutwa kucha.

Maendeleo ni mazuri lakini maendeleo yanapokuja na tukayavamia kiasi cha kuondoa utu wetu, basi maendeleo hayo yatakuwa yanaturudisha nyuma kiutamaduni na hata kiitikadi, maana zamani kabla ya haya mambo ya video kuingia na kuonyesha vilamu za mauwaji, ujambazi na laana za kila aina, watu tulikuwa tukilala usingizi, lakini tangia haya mambo ya Filamu za video kuzagaa sana mitaani na vijana wetu kuiga kila jambo walionao, uko mitaani kumekuwa uwanja wa vita, usingizi umepotea, ndio utakuta mtu anajenga nyumba kama gereza, milango nondo madirisha nondo, gate la chuma, mbwa na mlinzi juu, na bado akilala anaweweseka kuibiwa.

Sasa zimeingia hizi TV kwa ving’amuzi, hapo ndio kabisaa tena ukijumlisha na hizi playstation na xbox vijana wetu hata kutoka kwenda kucheza mpira viwanjani imekuwa hawaendi tena, kila kitu hapo hapo.

Mbaya zaidi kuna huyu mtaalam wa mambo yote, anajulikana sana kama intaneti akishirikiana na nduguye gugo dot komu, hapo ndio balaa, maana uko kuna kila kitu, watu siku hizi wamekuwa wajuwaji, maana hata kama kitu hakijui, mbio anabofya gugo anachukuwa makapi, chenga, mchele safi na pumba vyote anakusanya na kuvikumbatia. Tena wamekuwa mahodari sana, utawaambia nini na gugo yupo mwenye kujuwa kila kitu?

Haya maendeleo si mabaya kama utachunga mustakabari wetu na kuweka hishima kwa kila mtu tunayewasiliana naye, tukirisha utamaduni wa kusoma vitabu na kuwaenzi walimu wetu na waliotuzidi umri, hakika tutakuwa tumetunza hishma yetu mila na utamaduni wetu.
Tumerudi na msomi wangu,nilikuwa na mishemishe za kimaisha siku mbili hizi hivyo hatukupata muda wa kufunzana.
Leo tumeingia herufi D


Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!