20 November 2014

Mwanamke mmoja aliyejulikana kwa jina la Tatu Ikoko mkazi wa Mwananyamala jijini Dar, hivi karibuni alifunga mtaa kwa kutembea bila nguo baada ya kumfumania mumewe akiwa na mwanamke mwingine.

Chanzo chetu cha kuaminika kilisema mwanamke huyo aliondoka nyumbani kwake usiku wa Ijumaa iliyopita na aliporejea asubuhi, alimkuta mwenzake akiwa na kigori mwingine ndani ndipo alipopagawa.

“Alitoka usiku mzima akarudi saa moja asubuhi akamkuta bwana’ke yuko na mwanamke mwingine ndani,  akaanzisha vurugu, akavua nguo na kubaki na kanga moja na kuanza kupita mtaani huku akisema nivue nisivue na watu wakawa wanamuitikia vua.

“Baada ya hapo tu watu wazima na mashosti zake  walimshika na kumsitiri, akaja bwana’ke akamchukua wakaenda nyumbani kwao,” kilisema chanzo hicho.
Chanzo kiliendelea kufunguka kuwa tukio hilo siyo mara ya kwanza kwa mwanamke huyo kwani alishawahi kufanya hivyo akiwa na mwanamume mwingine aliyejulikana kama Kisiso mtaani hapo na waliachana kwa tabia hiyo.

“Akiwa na mwanaume halafu akamfumania, ndiyo huwa anafanya hivi na yule mshikaji wa kwanza kwa aibu ilibidi ahame, sasa hivi anaishi Mbagala,” kilisema chanzo hicho.

Imeletwaa na Shani Ramadhani & Mayasa Mariwata.
Reactions:

0 comments:

Post a comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!