21 November 2014

Hii Habri tumeletewa na Mdada na akatuomba tuiweke hapa ili wanawake walioko kwenye ndoa na wale ambao hawapo kwenye ndoa wapate kujifunza na kuchukuwa taadhari.

---
Naitwa Josephina (Si jina lake) mnaweza kushangaa kwa kuamua kuiweka habari hii kwenye mitandao ya kijamii. Lakini kwa mapenzi yangu nimeamua kukiweka kisa hiki ambacho kimenikuta kiwe funzo kwa wadada wote watakao bahatika kukisoma.

Kwa miaka mitatu mfurulizo nimekuwa katika matatizo makubwa sana kwenye njia yangu ya uzazi. Nawashwa sana ukeni, hospitali walisema kuwa nasumbuliwa na fungus.

Nikawa natumia dawa za aina mbalimbali na kila dawa imekuwa haileti matumaini ya aina yoyote. Kila nikitumia dawa baada ya wiki tatizo linarudi pale pale.

Nimekuwa mtu wa kujikuna muda wote, uchi unawaka moto kwa kujikuna. Nimeendelea na tiba mpaka likaibuka tatizo lingine jipya, kila ninapofanya tendo ndoa napata maumivu ambayo hayaelezeki. Wakati mwingine mpaka naanza ku-bleed.

Nikaona nirudi hospitali kwa vipimo zaidi ili kujuwa kinacho nisumbuwa haswa ni nini. Nikapima vipimo vya kansa, na wakatoa kinyama ndani na kufanya vipimo.

Baada ya wiki mbili majibu yakatoka, wakasema hakuna kansa ya aina yoyote. Lakini ajabu tatizo likawa linazidi kuongezeka na sasa siwezi tena kufanya tendo la ndoa.

Baada ya uchunguzi wa kina madaktari wakagundua kuwa ndani ya uke kwenye mlango wa kizazi kuna wekundu mwingi sana, usio wa kawaida. Badala ya rangi ya pink. kumbe ile rangi nyekundu ni sehemu ambayo inashambuliwa sana na bacterial wasio sikia dawa.

Wakajaribu kupeleka dawa hapo kwenye hilo eneo lililoathirika bado ilishindikana kuwaua walikuwa bado wanaonekana wanashambulia.

Ikabidi madatari muhimbili waniulize jinsi ninavyofanya usafi katika uke wangu.

Nikabidi niwaeleze ukweli nilichokuwa nafanya...!

''Huwa najisafisha kwa kuingiza vidole ndani kisha najiingiza Asali niliyoipaka kwenye pamba. Naingiza ndani ukeni ili Uke uwe umebana. Na vitu vingine vingi kama wasichana wengi tunavyo shauriana (VIUNGA KUMA)."

Madaktari wakaniambia sababu ya matatizo yangu yamesababishwa na hivyo vitu, vikiwemo Asali na manukato mengine. Bakteria wote ambao ni walinzi nimewaua kwa kuweka hivyo vionjo. Na ndio maana uke wangu unashambuliwa sana na bacteria ambao hawasikii dawa.

Ndugu zangu makungwi wenzangu, leo hii nalia peke yangu nilikuwa nikiunga sana uke wangu kwa viungio na naingiza vidole vyenye kucha ndefu wakati mwingine nikiingiza mpaka sabuni ili kijisafisha.

Ili kuokoa maisha yangu Madktari wamesema ni lazima wanitoe kizazi changu, sababu nikiacha itageuka na kuwa kansa.

Hali yangu ni mbaya kwa kweli na mimi bado binti mdogo natolewa kizazi nikiwa na miaka 29 tu.

Natarajia hivi karibuni kufanyiwa operation ya kutolewa kizazi. Naomba sana mniweke katika sala zenu ili operation iende salama...!

Nawapenda wote!
Reactions:

0 comments:

Post a comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!