31 January 2015

Je unaogopa kuvaa hijab,unaogopa watu watakuchukuliaje unapovaa hijab?
Asalam alykum warahmatullah wabarakatuh.
Ndugu zangu wanawake katika Imani, ambao mnahofia kuvaa hijab,labda kwa uoga,Aibu ya kuonekana mpo nyuma kimitindo,kuhofia kuchekwa kwa kuvaa  hijab?Binafsi nafahamu nini mnawaza/unawaza kuhusu suala zima la kuvaa hijab,nami nilitokea huko(kama utakuwa ulisoma makala yangu ya mwaka jana)
Nikurudishe nyuma kidogo nilianza kuvaa hijab mwaka 2011 mara baada ya kwisha ramadan kwangu ni hatua kubwa sana nilichukua na alhamdulillah hijab ni moja ya rafiki wangu wa karibu sana.

Nikupe muendelezo mfupi wa maisha yangu na hijab yangu...mimi ni mwanachama wa network moja inaitwa fingal ethnic network katika viongozi wa network tupo wanawake wawili tu.
Siku moja tukiwa katika kikao pini yangu ya hijab ilifunguka sikujali sababu ndani nilikuwa nimevaa kitambaa kingine,sasa ikafika wakati wa kupiga picha nikasimama nikafunga hijab yangu vizuri ili niende katika picha,mmoja wa member mwenzangu ambae ni mwanaume akasema kwa sauti ya juu kabisa Mammy ninapenda sana huo utamaduni wako,yaani mimi sio muslim ila ninakuthamini na ninapenda unavyovaa hiyo skafu yako.
Ndugu yangu mwanamke unasubiri kutoanza kuvaa hijab yako upate thamani mbele ya jamii

Ushauri wangu 
Unapotaka kuanza kuvaa hijab,Kwanza katika kichwa chako ondoa fikra zote potofu kuhusiana na watu/rafiki zako watakavykuchukulia kwa kuvaa kwako hijab,usiogope kabisa ,kuwa muwazi kifikra kuhusiana na tofauti zote za watu wanaokuzunguka wakavyoanza kuongea kwa wewe kuvaa hijab,kwani utakapokuwa umeanza kukubaliana na mitazamo yao juu ya kuvaa kwako hijab,itakuwa tayari umeshaozoea na kuipenda hijab yako,
Usikubai kuyumbishwa,jidhatiti na jiamini pale unapokuwa umevaa hijab yako,kwani huwezi kukabiliana na yote watakayo kuwa wanayazungumza kwa wewe kuvaa hijab,na hili lisikuogopeshe kabisa sababu litakuwa la muda mfupi na watakuzoea na kupenda uvaaji wako wa hijab,hivyo unaweza kuyasahau yale yote waliyokuwa wakiyaongea kuhusu wewe.
Nakuahidi wale wote walikuokuwa wakikuona kwa uvaaji wako wa hijab wewe ni mshamba,upo nje ya mitindo basi ni hao hao watakaonza kukusifia.
Binafsi nilipogundua hili ilikuwa rahisi kwangu sana.
Amini najua nini unawaza kuhusiana na wewe kuanza kuvaa hijab,haupo peke yako,kila mwanamke/msichana aliyetaka kuanza kuvaa hijab alikutana na vikwazo na mawazo hayo,hata mimi ilikuwa hivyo ila alhamudillah imeweza na nazidi kumuomba mwenyezimungu aniongoze katika uvaaji wangu wa hijab.
Pigana na mawazo yako,jiamini kuwa unaweza na hakuna wakukukatisha tamaa ya kuvaa hijab,wachukulie kama ni ibilisi wabaya nafahamu utaweza kuvaa hijab yako na ukapandeza.





2 comments:

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!