11 October 2012


Afisa Mtendaji Mkuu wa Kampuni ya Kidoti Jokate Mwegelo akizungumza wakati alipozindua rasmi kampuni hiyo inayojishughulisha na Uuzaji wa Nywele za Style mbalimbali Ubunifu wa mavazi ambapo ameongeza kuwa nywele hizo zimejaribiwa na kukidhi matakwa ya kudumu, kuweza kutumiwa tena na tena, uzito pamoja na msokotano na zitakuwa zikipatikana katika mitindo na urefu mbalimbali zitazotumiwa na wasichana na kinamama.
Ameongeza kuwa Nywele hizo pia zitawafikia watu wa mikoani pia.

Afisa Mkuu Mtendaji wa Kidoti Jokate Mwegelo akitambulisha timu ya watu anaofanya nao kazi katika Kampuni yake kwa waandishi wa habari na wageni waalikwa.
Pichani Juu na Chini ni Models wakionyesha aina tofauti za Nywele za Kidoti zinazotengenezwa na Darling Tanzania.
Selita Style.
Hii ni aina ya Nywele inayoitwa Jokate,
Aina ya Nayomi.
Models katika picha ya pamoja mbele ya wageni waalikwa.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Kidoti Peter Kasiga akielezea ubora wa Nywele hizo na bei zake kwa wageni waalikwa na wandishi wa habari waliohudhuria uzinduzi huo leo jijini Dar es Salaam.
Meneja Masoko wa Kampuni ya Kidoti Peter Kasiga pamoja na CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo wakijibu maswali kwa waandishi wa habari wakati wa uzinduzi huo ambapo pia amefafanua kuzinduliwa rasmi kwa tovuti ya kampuni hiyo leo itakayopatikana kupitia anuani ya www.kidotiloving.com
CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo katika picha ya pamoja na Models waliovaa nywele za Sanisi za Kidoti.
CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo katika picha ya pamoja na timu ya wafanyakazi wa kampuni yake. Kushoto ni Meneja Masoko Bw. Peter Kasiga, Operation Manager wa Faith Lukindo (katikati), Meneja Biashara Bruce Paschal (wa pili kushoto) na Meneja Mauzo Charles Benson.
"Ainisha Urembo Wako" by Jokate Mwegelo.
Pichani Juu na Chini ni Baadhi ya wageni waalikwa na wadau wa tasini ya urembo waliohudhuria uzinduzi huo uliofanyika jijini Dar es Salaam leo katika Hoteli ya Serena.
CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo akiwa na mbunifu nguli wa mavazi Khadija Mwanamboka a.k.a Kubwa la maadui.
Jokate Mwegelo akimpiga busu Khadija Mwanamboka kama ishara ya kumushukuru baada ya kuhudhuria uzinduzi wa kampuni yake.
CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo katika picha ya pamoja baadhi ya marafiki waliojumuika naye katika uzinduzi wake. Katikati ni Mdau Calvin na Fashionista Bella all the way from UK.
Jokate Mwegelo akishow love na Binamu yake Esi Sebastian na Mdau William Maelecela a.k.a Lemutuz.
Jokate Mwegelo na Cousin Sister wake Esi Sebastian.
CEO wa Kidoti Jokate Mwegelo akiwa na mmoja wa mawakala wake Said Rundika mwenye duka la Jumla Kariakoo mkabala na kituo cha Mafuta cha Big Bon eneo la Msimbazi.
Jokate Mwegelo na rafiki yake kipenzi Bella.
Kidoti ambayo ni chapa halisi ya Kitanzania imezinduliwa rasmi leo jijini Dar es Salaam.
Chapa ya Kidoti imeundwa katika taswira yake mwenyewe Jokate.
Sifa zake alizohakikisha zinaonekana kupitia Kidoti ni pamoja na akili, ujasiri, dhamira, yenye kuthubutu lakini pia yenye bashasha zote za kike.
Kidoti haitaishia katika mavazi na mitindo tu.
Kidoti ni harakati na mwanzo wa chapa ya mitindo-maisha yenye nia kuu ya kuwezesha kizazi change,” aliongeza Jokate.
Nywele sanisi za Kidoti ambazo zimezinduliwa leo katika soko ni zenye ubora wa hali ya juu zikiwa zimejaribiwa na wateja wake watarajiwa wenyewe.
Mtiririko mzima wa ubunifu na uzalishaji wa bidhaa hizi ulisimamiwa na kuongozwa na Jokate ambapo kila nywele zimejaribiwa na kukidhi matakwa ya kudumu, kuweza kutumiwa tena na tena, uzito pamoja na msokotano.
Nywele hizi zinakuja katika mitindo na urefu mbalimbali ambayo imebeba sifa za chapa hii zikiwa na mawimbo nyororo kwa ajili ya wanawake wanaopenda kupendeza bila kufilisi mifuko yao.
Pamoja na ubora wake wa hali ya juu, nywele hizi zinaendana kabisa na nia ya Kidoti ya kuvuruga na kuleta maana mpya katika tasnia ya mitindo kwa ubunifu wa kuweza kutengeneza mitindo mingi kutumia nywele moja na sifa hii inawasilishwa kwa soko walengwa kibunifu kupitia kasha za bidhaa hizi ambazo zimesheheni picha za Jokate mwenyewe akionyesha mitindo mbalimbali kwa ajili ya kila nywele. Sifa hii ya kipekee pia inawasilishwa kupitia maneno “nywele moja staili kibao!” yaliyochapishwa katika kila kasha.
Nywele za Kidoti zitapatikana kwa bei nafuu kupitia mawakala mbalimbali wa jumla na rejareja jijini kuanzia leo na zitauzwa kwa kati ya Sh. 9,500 na 12,000.
Mawakala hawa ni pamoja na maduka ya jumla na rejareja Kariakoo, saluni mbalimbali jijini na mtandao wa mawakala mikoani utakaokuwa na bidhaa zetu kuanzia wiki ijayo.
Nguo za Kidoti zitatambulishwa rasmi katika soko mwakani (2013) zikifuatiwa na vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.
Harakati ya Kidoti inaendeshwa na timu ya vijana wabunifu pamoja na kwamba shughuli za Kidoti zinaendeshwa kutoka Dar es Salaam, chapa hii ni ya kiulimwengu zaidi.
Chapa ya Kidoti ilianzishwa mwaka 2011 na Bi. Jokate Mwegelo ambaye ni mmoja wa watu mashuhuri nchini, kwa nia ya kubadilisha mtazamo mzima wa tasnia ya mitindo. Chapa hii itasheheni bidhaa mbalimbali zikiwemo nywele za sanisi ambazo zimezinduliwa leo pamoja na chapa. Bidhaa nyinginezo ni pamoja na nguo, vifuasi vya urembo pamoja na vipodozi.
Kidoti ni chapa yenye uwezo wa kubadilisha jinsi tunavyoichukulia tasnia ya mitindo hivi sasa.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!