27 November 2014


Elimu ndio njia pekee ya kuwalinda wanawake na wasichana dhidi ya "kitendo cha kinyama cha ukeketaji" 

Wasichana na wanawake wengi Kaskazini mwa Tanzania wamefanyiwa ukeketaji unaofahamika kama tohara ya wanawake, kwa mujibu wa ripoti ya mwezi Juni 2013 iliyoandaliwa na Shirika la Watoto la Umoja wa Mataifa (UNICEF).

Utafiti huu umebaini mazingira ya kutisha kuhusiana na sababu zinazochangia ukeketaji. Pamoja na mila na desturi, umaskini pia umeibuka kama sababu inayozisukuma familia nyingi kukeketa watoto wao ziweze kujiongezea pato kiuchumi.

Mkoani Mara, kabila la Wakurya ndio wenye ukwasi mkubwa kutokana na ufugaji. Wakurya kwa upande wao, wameweka viwango vya aina ya mwanamke wanayetaka kumuoa. Kwa Wakurya mwanamke ambaye hajakeketwa, si mwanamke wa kuolewa. Kwa nia ya kuendeleza mila hizi, Wakurya wanatumia ukwasi wao kuongeza idadi ya ng’ombe wanaotolewa kama mahari kwa binti aliyekeketwa, hali inayoshawishi makabila mengine mkoani Mara kukeketa mabinti wao waweze kutolewa mahari kubwa na Wakurya.
Mikoa ambayo imekithiri sana kwa Ukeketaji ni, Mkoa wa Mara, mkoa wa Kilimanjaro, Ukiwemo Moshi na Arusha, Singida, Irangi na Dodoma.
Ingawa uungaji mkono wa mila hiyo unapungua, lakini kazi kubwa inahitajika katika kuelimisha jamii mbalimbali za kikabila.
Nchi za Kiafrika zinazo ongoza kwa Ukeketaji ni Misri, Ethiopia, Somalia, Djibouti na Nigeria ndizo nchi zenye idadi kubwa zaidi ya wanawake wanaofanyiwa ukeketaji.

Ukeketaji si mila ya kidini, ni kitendo cha kuogofya ambacho kwa ufupi ni unyanyasaji dhidi ya haki za kibinadamu za wasichana. Tuwe wazi kabisa, hili ni jambo ambalo halikubaliki kabisa na tendo ambalo linatakiwa liwe ni kinyume cha sheria za nchi, na linapaswa liwemo kwenye katiba ya nchi.

Ni wakati sasa wa kuongeza nguvu na kuelimisha wazee wa koo za kikabila kubadilisha mitazamo na kuwalinda wanawake nchini dhidi ya ukeketaji."

Tudhamirie haswa kukomesha tabia hii mbaya na isiyokubalika dhidi ya wasichana. 

Serikali ishirikiane na wanaharakati wa kijamii kupitia taasisi zake Kutoa elimu na njia mbadala za maisha kwa wafanyao ukeketeji na pia kushirikiana na viongozi wa kijamii kuhamasisha watu juu ya madhara ya muda mfupi na mrefu yanayosababishwa na ukeketaji.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!