23 August 2014

Watu watatu, ikiwa ni pamoja na mtoto mchanga, waliuawa siku ya Alhamisi asubuhi (tarehe 21 Agosti) wakati watu wawili wenye silaha kurusha kifaaa cha kulipuka ndani ya basi la abiria katika wilaya ya Kasulu mkoa wa Kigoma, gazeti la The Citizen la Tanzania liliripoti.

Abiria wengine sita walijeruhiwa katika shambulio hilo, ambalo lilitokea karibu kambi ya jeshi ya Migongo katika wilaya ya Buhigwe. Majeruhi walihamishwa katika hospitali ya eneo hilo kwenda katika hospitali moja ya Kasulu Mjini siku ya Alhamisi mchana baada ya hali zao kuzorota.

Polisi walisema kwamba basi ilikuwa likisafiri kutoka Kilelema kwenda Kasulu Mjini wakati mtu mwenye silaha alisimama katikati ya barabara katika jaribio la kulizuia basi hilo. Wakati dereva alipokataa kusimama, mtu alikwepa, na wakati basi likikimbia, mtu wa pili alirusha bomu ndani ya basi, gazeti la The Guardian liliripoti.

Mkuu wa Polisi wa Wilaya ya Buhigwe Frank Utonga alisema kuwa washukiwa hao hawakuchukua chochote kutoka kwa abiria.

"Kwa sasa tunachunguza tukio hilo na tutatoa ripoti," alisema. "Tunataka kujua kwa nini walitekeleza misheni hiyo."

Mkurugenzi wa Uchunguzi wa Makosa ya Jinai Issaya Mngulu aliiambia The Guardian kwamba mwezi uliopita kwamba mfululizo wa mashambulizi ya mabomu ya hivi karibuni nchini kote yanaandaliwa na mtandao wa ndani wa makosa ya jinai, na sio mitandao ya kigeni ya makosa ya jinai kama inavyovumishwa.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!