6 June 2012



  • Athuman Khamis, alipokuwa akirejea toka kwenye matibabu.

    Ndugu zangu wapendwa, ninawasalimu katika jina la tunayeamini kuwa ndiye mwenye kutuweka hai humu duniani pamoja na kutuwezesha kwa kila kitu tunachokifanya katika kuendeleza maisha yetu ya kila siku.Pamoja na kuwa mikakati ya kuanzisha tmark-turn family ipo njiani,lkn ninaamini wale wote wanaopita na kusoma habari ziandikwazo humu ni familia ya tmark-turn.kundi hili pamoja na blog zetu.Na ndio sababu nimeona mahali hapa ni sehemu murua kabisa ya kufikisha ujumbe kwa wasomaji na wapenzi wote wa tmark-turn blog,katika suala hili linalomuhusu mmoja wa mwanataaluma mwenzangu.
    Ndugu zangu, hakuna asiyejua mazingira ya wafanyakazi wa Kitanzania inapotokea amekumbwa na matatizo kama yaliyomkumba ndugu yetu Athuman, lakini naamini hakuna asiyejua kuwa hali inakuwa mbaya zaidi hasa pale inapotokea kuwa mhusika ni mwanataaluma ya uandishi kwani mazingira ya kazi zetu yanajulikana. Hakika inasikitisha na kuhuzunisha. Na Mungu atulinde sie/na wanataaluma wengine atuepushe na haya yaliyomkumba mwenzetu Athuman Khamis.
    Baada ya kuusikia mkasa wa kaka yetu huyu, binafsi niliguswa na matamshi yake na nikawaza haraka sana niwe mtu wa kwanza kumchangia. Lakini nikakumbuka kuwa, kuna ndugu, jamaa na marafiki zangu ambao tupo nao katika jamii inayotuzunguka, ambao niliona ni vyema nikawashirikisha ili kwa yule mwenye nia, basi tuungane kusudi kile kidogo changu na kidogo chako, kiweze kuwa kikubwa na kumpa msaada ndugu Athuman.

    Ni vigumu sana kuweka malengo kuwa tufikie wapi, lakini ni vyema ikawa wazi kuwa, kutoa ni moyo na wala si utajiri. Na katika hili, ninapenda kuwaomba wasomaji wa tmark-turn   kuungana nami katika kufanikisha lengo la kuchanga kiasi chochote tunachoweza kuchanga ili tukiwasilishe kwa ndugu yetu kama ishara ya kuonyesha kuwa tuko naye katika wakati huu wa matatizo yake.

    Ikiwa unaguswa na hili, tafadhali usisite kuwasiliana Rama S.Msangi  kupitia anwani zake  za barua pepe 
    msangirs@jukwaahuru.com, info@jukwaahuru.com
    au simu namba +255784412176.  milango ya kupokea michango hadi tarehe 28, ili ifikapo tarehe 30 ya mwezi huu,michango yote itawakilishwa kwa muhusika,hii ni kwa wasomaji wa blogs,na wamiliki wa blog
    Msaada huo pia unaweza kupeleka moja kwa moja kwa muhusika kwa akaunti namba za CRDB, 01J2027048800, Posta Benki namba 010-00090488 na kwa namba za mitandao ya simu za M-Pesa 0757825737, Tigo-Pesa 0655531188, Airtel Money 0784531188, M-pesa ya Chris Mahundi 0767298888 na Airtel Money ya Ephraim Mafuru namba 0686710977.
    Mpango huu wa hiari hakika halazimishwi mtu yoyote kuchangia,zisije zikatolewa lugha zisizo nzuri samahani sana. 
Categories:

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!