14 January 2014


Msajili wa kwanza wa vyama vya siasa nnchini Tanzania , Jaji Mstaafu George Liundi, amefariki Dunia nyumbani kwake eneo la Keko, Dar es Salaam, akiwa na umri wa miaka 76.

 Taarifa ya kifo cha Jaji Liundi zimetolewa na mtoto wake, Taji Liundi (Master T), ambaye anafanya kazi kwenye shirika la utangazaji TBC1, baba yake alifariki muda mfupi baada ya kulalamika maumivu ya mgongo walipokuwa wakimpeleka hospitali.

Taji Liundi, alivitaarifu vyombo mbalimbali vya habari kuhusiana na msiba huo kwa kusema kwamba siku tatu zilizopita baba yake alikuwa alilalamika maumivu ya mgongo. Ilipofika majira ya mchana siku ya Jumapili marehemu aliomba achuliwe na vipande vya barafu ili kupunguza maumivu, lakini hata hivyo hali haikuwa nzuri.

Mida ya saa sita mchana hali ilikuwa mbaya zaidi na kiasi cha kupelekea mgonjwa kupoteza fahamu na kuzimia, marehemu akakimbizwa hospitali ya TMJ Mikocheni, lakini hawakuwahi kufika hospitali na mgojwa akaaga dunia wakiwa kona ya Morocco.

Marehemu Jaji Liundi, alizaliwa kijijini Chitowe wilayani ya Masasi, mkoani Mtwara mwaka wa 1938, atazikwa siku ya Alhamisi na kufuatilia na Misa fupi uko nyumbani kwake  Keko.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!