Unapoingia kwenye majumba ya waislam wengi si jambo la kushangaza kukuta Luninga (TV) varandani na wakati mwingine mpaka vyumbani, kwenye vyumba vya kulala.
Watoto wetu wa siku hizi wamekuwa kama mazombi (mandondocha), hawana utulivu tena na luninga ndio imekuwa kibembelezi kwa watoto wanao tusumbua au kulia lia pale tunapokuwa na maongezi au jambo ambalo linaitaji usikivu.
Lakini hali hii si kwa watoto tu, hata watu wazima, maana hao ndio kabisa wamekuwa mandondocha (Zombies), unaweza kumkuta mtu anashangalia TV hata habari hana, swala zinampita, majukumu yake ndani ya nyumba yanampita, yeye yupo kakodolea macho michezo ya tamthilia, mashindano ya mpira na michezo mingine isiyo na maadili, yaani luninga ndio zimekuwa Qibla kipya kwa Waislam wa karne hii.
Watu wengi ujiona hawajakamilika kama ndani ya nyumba hakuna Luninga na ujiona kama washamba au hawajaendelea, sababu tu hakuna Qibla kipya cha kukielekea.
Ile hali ya kuishi kifamilia ndani ya nyumba miaka hii imepotea kabisa, watoto hawachezi tena nje, wakitoka nje basi wanataka kuiga yale walio ona kwenye luninga, wazazi nao hawapo nyuma, fasheni za mitindo ya mavazi filamu na tamthilia kwenye luninga ndio zimekuwa masimulizi ya kila siku kwenye simu na mazungumzo ya kawaida wanapo kutana.
Wataalam wa saikolojia wanatuambia kuwa Mtu mzima/mtoto anayetumia saa tatu na zaidi kwenye luninga kila siku kuna uwezekano wa kupoteza utulivu na umakini darasani au katika kazi zake. Na hii inasababishwa na ile michezo inayotolewa kwenye vipindi vya luninga na kuchota mawazo na akili kiasi cha kusababisha pumbao na ustarehevu wa muda kwenye akili ya binadamu.
Na inapotokea mtu au mtoto kukosa zile pumbao, basi akili yake inakosa utulivu na ujiona mchovu na upoteza hali ya uchangamvu na umakini katika jambo analotaka kulifanya.
Sina maana ya kuwakataza watu wasitazame Luninga lah hasha, tunaweza kutazama haswa kama vipindi vitakuwa na mafundisho na faida kwetu na haswa vipindi vya dini, taarifa za habari na vipindi vya kimaendeleo nakadharika.
Lakini tutakapoigeuza Luninga (TV) kuwa ndio Qibla chetu, hapo ndio tutakuwa tumepotea na kukipoteza kizazi chetu, maana tutakuwa tunaangalia kila kinachojili kwenye luninga, kiwe chenye maadili au lah. Na kisha tunashangaa kuwa watoto zetu wana tabia za ajabu ajabu na tunashangaa wapi wamezipata, kumbe ni kile Qibla kipya tulicho kinunua kwa pesa nyingi na kukitafutia nafasi nzuri varandani kwetu.
Unatarajia Mtoto/Watoto Watakusikiliza Kweli Wakati Katuni wanazo Tazama Ni Hizi...!
• Tarzan: Maisha yote anaishi Nusu UCHI
• Cinderella: (Kisonoko) kila leo anakirudi nyumbani usiku wa manane.
• Pinokio: UONGO wakati wote.
• Aladdin: ni MFALME WA WEZI.
• Batman: anaendesha gari mbio kwa Mwendo kasi wa 200 mph.
• Romeo & Juliet: WALIJIUWA Kwa Sababu ya MAPENZI.
• Harry Potter: Anatumia UCHAWI.
• Mickey & Minnie: Ni zaidi ya MARAFIKI.
• Sleeping Beauty: Msichana MVIVU.
• Dumbo: Ni MLEVI.
• Scooby Doo: Kla siku yeye na Ndoto za MAJINAMIZI.
• Snow White: ANAISHI NA WANAUME SABA Chumba kimoja.
Hatupaswi Kushangaa Wanapokosa ADABU. Kwa sababu wanajifunza Tabia na Mienendo kutoka kwenye vipindi vya katuni kwenye Luninga na Vitabu vya hadithi za Watoto, ambavyo maadili yake hayaendani na Uislam.
Tunapaswa badala yake kuwa kuwafundisha simulizi za Maswahaba wa Mtume (saw) kama vile:
• Abu Bakr (ra) alivyokuwa ni Muaminifu, Kweli na Muadilifu.
• Umar ibn Khatthab (ra) Uvumilivu, Upendo kwa ajili ya kutetea HAKI.
• Uthman ibn Affan (ra), Haya na Staha.
• Ali ibn Abi Talib (ra) Ujasiri na Ushujaa.
• Khalid ibn Waleed (ra) Tamaa ya kupambana na Maovu.
• Fatima bint Muhammad (ra) Upendo na Heshima kwa baba yake.
• Sallahuddin Al-Ayubi (rh) Shujaa aliye Ikomboa Jerusalem.
Na Mengine Mengi Mazuri kutoka Kwente Historia (Tarekhe) ya Kislam...
Zaidi ya yote...
Tunapaswa kuwafundisha juu ya kumpwekesha MwenyeziMungu (swt), Kusoma Qur'an na Sunnah za Bwana Mtume (saw).
0 comments:
Post a Comment