15 December 2013

Peter O'Toole, Nyota wa Sinema ya Lawrence of Arabia, amefariki akiwa na Umri wa miaka 81

Familia ya Mwigizaji Lawrence of Arabia, wametangaza kuwa Marehemu alikuwa akisumbulia na saratani ya tumbo kwa kipindi kirefu sana, tangia mwaka 1970. Marehemu alikuwa amelazwa kufia katika Hospitali ya Wellington jijini London.

Mtoto wake wa Kike Kate O'Toole amesema kuwa : "Familia yake inatoa shukran za dhati na upendo wa kweli kwa ndugu na jamaa wote kwa kipindi chote cha ugonjwa wa baba yake mpaka kufariki kwake.

O'Toole alitangaza kuacha kuigiza na kuamua kustaafu moja kwa moja mwaka 2011

Peter O'Toole alimwoa Siân Phillips mwaka 1959 na wakatengana mwaka 1979, walijaaliwa kupata watoto watatu, Kate O'Toole, Patricia O'Toole na Lorcan O'Toole.

Filamu iliyompa sifa ni ile ya Lawrence of Arabia ya Mwaka 1962.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!