16 December 2013



Nyumba ya familia moja huko mtaa wa ugombolwa Kata ya Segerea ikiwa inateketea kwa moto usiku huu mara baada ya Baba wa familia hiyo kuhisi kuwa mke ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mmoja na kuamua kuichoma moto nyumba hiyo sababu ya wivu wa mapenzi.
Nyumba ikiendelea kuteketea kwa moto mkali
Kwa moto huu hakuna kilichoweza kuokolewa mpaka sasa
Baadhi ya Wakazi wa Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea Wilaya ya Ilala Jijini Dar wakishuhudia nyumba hiyo ikiteketea kwa moto.
Segerea, Dar Es Salaam, Nyumba moja iliyopo Mtaa Ugombolwa Kata ya segerea Jijini Dar imeteketea kwa moto mara baada ya baba wa familia ya nyumba hiyo kuhisi kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine. 

Hali hiyo imetokea usiku huu majira ya Saa tano Kasoro usiku katika Mtaa wa Ugombolwa, Kata ya Segerea, Wilaya ya Ilala Jijini Dar Es Salaam ambapo inasemekana baba wa familia hiyo alichukua uamuzi huo mara baada ya kusikia kuwa mkewe ana mahusiano ya kimapenzi na mwanaume mwingine nje na mara baada ya kutokuelewa kwao ndipo alipochukua uamuzi huo wa kuitia moto nyumba hiyo.

Mmoja wa shuhuda alisikika akisema kuwa "Hawa Wachaga wana matatizo sana Ebu Ona Sasa mwanaume Mzima Anateketeza Nyumba yake aliyoijenga kwa mamilioni ya Shilingi kisa Mkewe anatembea nje ya ndoa Sasa ona watoto wake wataishi wapi?..watu wengine ni wajinga sana Kama mwanamke anatembea nje ya ndoa si umpe talaka tu" alisikika akiongea Shuhuda huyo.

Mpaka Mtandao huu unaondoka eneo la tukio nyumba hiyo ilikuwa bado ikiteketea kwa moto na hakuna dalili zozote zile zilizokuwa zikichukuliwa kwaajili ya kupambana na moto huo huku ikiwa haijafahamika kama wakati nyumba hiyo ikitiwa kiberiti familia ya huyo baba ilikuwepo ndani ya nyumba au laah huku ikikadiriwa kuwa mali zote zilizomo ndani ya nyumba hiyo zimeteketea kwa moto kwani mpaka tunaondoka hakuna kikosi cha zimamoto kilichofik eneo la tukio wala majirani hawakuonyesha dalili zozote zile za kuuzima mot huo.

Mpaka tunaondoka eneo la tukio hakuna taarifa yoyote ile ya majeruhi wala watu kupoteza maisha katika ajali hiyo ya moto.

Source: Jamii Forum



0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!