15 June 2012


Wema akiwa ndani ya mjengo wake.

Kwa mujibu wa chanzo kisicho na shaka ambacho ni mmoja wa mashosti wa Wema, wamedai nyumba iliyosemekana ni ya Wema Sepetu anayotarajia kuhamia hivi karibuni ipo Mtaa wa Bwawani, Kijitonyama jijini Dar es Salaam sio ya kwake.

MADAI MABICHI
Kikifichua mambo mazito nyuma ya pazia, chanzo hicho kilidai kuwa watu wanaoijua ishu hiyo kiundani walipigwa na butwaa waliposikia Wema anamiliki mjengo huo wa kifahari huku wao wakielewa vingine.
“Ninavyojua ile nyumba siyo yake bali amepanga tu,” kilidai chanzo hicho na kuongeza:
“Aisee! Nimeshangaa kusikia Wema kanunua lile jumba wakati mchakato wa kwanza wakiwa na madalali walikuwa wakitafuta nyumba ya kupanga.
“Kusema kweli jambo lililonishangaza ni kuwa mpaka mchakato wa mwisho unafanyika kuhusiana na nyumba hiyo ni kwamba Wema alikuwa anaipangisha na siyo kuinunua.”

SIKIA HILI JIPYAAA
Wakati tukisikiasikia hayo, tukaletewa lingine jipya na sosi mwingine kuwa Wema alipewa jumba hilo lililokuwa likimilikiwa na mama Ngoma ili amalizie kurekodi filamu yake mpya ya The Superstar.
“Si mnakumbuka alivyofanya juzikati kwa kuvishwa pete ya uchumba na Mwinyi wa Machozi kumbe alikuwa anarekodi filamu, ndiyo hivyohivyo kwa hili jumba, kama hamuamini mtaona baadaye.
“Wewe angali vizuri hizo picha, ni za filamu kabisa kwani kipande cha hiyo muvi kinamtaka aonekane akiishi maisha ya kistaa sana. Wewe nyumba gani umetenga mpaka chumba cha kuzungumza na vyombo vya habari?” alihoji sosi huyo.

UTATA
Wakati mambo yakizidi kuwa mengi, kikaibuka chanzo kingine kikidai kuwa si kweli kwamba mjengo huo unamilikiwa na mama Ngoma bali ni ya Mwarabu fulani.
Baada ya kuambiwa vitu kibao kuhusu jumba hilo, Ijumaa lilianza kusaka ukweli ili kujibu maswali ya mashabiki wa Wema.

HUYU HAPA MENEJA WAKE
Mtu wa kwanza kuzungumza na Ijumaa ni meneja wa Wema, Martin Kadinda ambaye alikiri Wema kununua nyumba hiyo lakini si kwa Sh. milioni 400.
“Unajua huyo anayesema kuwa Wema amepanga siyo kwamba anakosea ila anachelewa kujua mambo.
“Ni kweli kabisa mara ya kwanza Wema alikuwa anataka kupanga nyumba hiyo lakini baadaye alikaa chini na mwenye nyumba na kukubaliana kufanya biashara ya kumuuzia lakini si kwa Sh. milioni 400,” alisema Martin.

MILIONI 400 KIVIPI?
Akifafanua fedha hizo zinazodaiwa kununulia mjengo huo, Martin alisema:
“Hiyo milioni 400 ni thamani ya nyumba na vitu vyote vya ndani. Siyo bei iliyonunuliwa.”

Kwa habari zaidi soma hapa GLOBAL PUBLISHERS INFO
Reactions:
Categories:

1 comment:

  1. WAT A NICE HOUSE, I LOVE IT.
    THATS WEMA I KNOW.

    ReplyDelete

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!