15 June 2012

Sheikh Farid Hadi Ahmed

Baada ya watanzania Visiwani kutokukubaliana na katiba iliyopo hasa juu ya mustakabali wa Muuangano,hali iliyopeleka kutokea na machafuko visiwani humo,kiongozi wa Jumuiya ya Uamsho ya Visiwani Zanzibar Sheikh Farid Hadi Ahmed,amefanya mahojiano na mwandishi wa gazeti la Jamuhuri bwana Manyerere Jackson.

Katika mahojiano hayo shekhe Farid amesikitishwa na kitendo cha serikali ya Tanganyika kuunga'ang'ania mji wa Dar es Salaam huku ikiwa inajua kuwa mji huo upo ndani ya visiwani hivyo kwa maili kumi huku akisisitiza kuwa mikataba inayoonyesha mji huo upo ndani wa visiwa hivyo ipo.

Ameeleza pia lengo kuu la mihadhara waliyokuwa wakiifanya,si kuleta fujo,bali nikutaka kuwaelimisha wananchi juu ya mustakabali wa muungano na katiba kwa ujumla.
Yafuatayo ni mahojiano ya mwandishi Manyerere na kiongozi wa wanajumuiya ya UAMSHO Shekh Farid 

JAMHURI: Ni nini chanzo cha vurugu za Mei 26?
Sheikh Farid: Kilichotokea hapa kwa muda mrefu, japo inasikika Jumuiya ya Uamsho ndiyo inayofanya mihadhara, lakini ni Umoja na Jumuiya za Kiislamu ambazo zimekuwa zinaendesha mihadhara. Tumefanya mihadhara zaidi ya mia moja hadi sasa – mikutano zaidi ya mia pamoja na makongamano tofauti. Na lengo zaidi hapo awali lilikuwa ni kuwaelimisha watu kujua Sheria ya Mabadiliko ya Katiba na kuona ni jinsi gani inawabana Wanzibari na haijawapa ile haki yao ya kuujadili Muungano.

Na baada ya hapo kilichokuwa kinazungumzwa zaidi ni kuwaelimisha wananchi kujua haki yao kujua mustakabali wa nchi yao na umuhimu wa kuuhoji Muungano au kuujua Muungano. Wazanzibari wao kama washirika na Watanganyika wana haki ya kuuhoji Muungano. Sasa hii mihadhara imeendelea kwa muda mrefu na ilikuwa inakwenda misafara ya mbali mingine hadi shamba. Na ilikuwa misafara mikubwa inaweza ikabeba magari mia mbili, mia mbili na zaidi, kuna mapikipiki, watu wanakwenda wanarudi kwa usalama wala hakuna tabu na matatizo yoyote. Hayo yote ndiyo kwa jumla yamefanyika.

Sasa kilichojitokeza hivi karibuni ni kuwa lilifanyika kongamano. Katikati ya lile kongamano watu waliamua kutembea, kama ni matembezi tu lakini si maandamano hasa. Maandamano ni kitu ambacho kimeandaliwa, kina slogan yake, kina ujumbe, kinaenda maeneo maalumu kufikisha ujumbe maalumu. Haikuwa hivyo.

JAMHURI: Je, Polisi walivamia?
Sheikh Farid: Polisi hawakuvamia, hawakuwahi kuvamia. Na walipokuja kwa kweli walikuja matembezi yameanza kutoka maeneo ya Lumumba. Watu wote wameacha baiskeli zao, vifaa vyao palepale na walinzi walibaki eneo lile. Watu wametoka wametembea mpaka hapa Michenzani, katika roundabout, wameshuka chini mpaka maeneo ya Kariakoo. Kwa hiyo watu wakaenda moja kwa moja wakarudi kwenye kile kiwanja walichoanzia. Wakarudi palepale wakaaa kitako. Wakawa wanaendelea na shughuli zao. Wakazungumza, wakazungumza mpaka wakamaliza. Walipomaliza kuzungumza wakatawanyika wakaenda majumbani mwao salama salmini.
Categories:

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!