25 September 2012


  1. HIVI NDIVYO ALIVYOANDIKA HAPPY KATABAZI KATIKA PAGE YAKE YA FACEBOOK,KUHUSIANA NA MAREHEMU AGNES YAMO

    Marehemu Agnes Yamo

    Agnes Yamo,mdogo wangu sisi tulikupenda ila mungu amekupenda zaidi.Jana kuanzia saa sita mchana mimi na mama yangu tulikupokea pale Hospitali ya Jeshi Lugalo,ukiwa huna fahamu na madaktari na manesi wa Lugalo walijitahidi kadri ya uwezo wao...
    kuokoa maisha yako bila mafanikio.Jana saa 12 jioni manesi wa hospitali hiyo walitupatia vipimo walivyomchukua Agnes wakitaka twende Hospitali ya Mhimbili tukavipime na kisha tuwaletee majibu na kweli mimi na kaka wa Agnes, Injinia wa JWTZ, Samwel Yamo, tuliamua kwenda maduka ya madawa Kawe na kununua dawa moja na kisha kwenda kwenye Mahabara ya Hospitali ya Mhimbili kwaajili ya kupima vile vipimo zaidi ya vitano na pale tulikaa pale Mhimbili na kupatia majibu yetu na ilipofika saa mbili usiku tukaanza safari ya kurudi Lugalo,na tulipofika Lugalo saa tatu suki mimi na Samwel tulikabidhi majibu ya vipimo hivyo kwa manesi na kidogo tulimkuta Agnes akianza kupata nafuu kwa mbali huku akiwa ametundikiwa Drip la Damu.Kumbe jana saa nne usiku mimi, mama yangu na ndugu zao pamoja na kaka yako Sam tulipokuwa tunazungumza na wewe wodini ukiwa umeanza kupata fahamu kwa mbali na ukaanza kuongea na Ishara,huku ukiwa unamngang'ania mama yangu Oliva asiondoke kwenda nyumbani alale na wewe kumbe ndiyo ulikuwa unatuaga kwa mara ya mwisho.Sisi tuliondoka usiku huu tukiwa na matumaini makubwa kuwa angalau umeanza kupata nafuu ukilinganisha na jana mchana wakati unaletwa hospitalini hapo kumbe ndiyo ulikuwa unatuaga.Na leo asubuhi ndio mama yangu ananipigia kumuuliza hali yako mama ananificha ananitaka mimi na bossi wetu Absalom Kibanda twende kwanza Lugalo hadi pale nilipoaza kuzungumza na mama kwa ukali anieleze unaendeleaje ndipo mama akaanieleza ukweli kuwa umefariki na Kibanda naye ambaye alifika asubuhi ya leo Hospitalini hapo naye akanipigia simu kunithibitishia kuwa umefariki.Nilisikitika sana na kuanza kulia mwenyewe.Agnes alikuwa ni mdogo wangu ni kitaaluma kwani nilimpokea alipoanza kazi pale Habari Corporation mwaka 2004,nilimfundisha jinsi ya kusaka habari na kumuunganisha na vyanzo kadhaa vya habari, lakini mwanzoni mwaka mwaka 2005 Agnes alipunguzwa kazi hapo na alikuwa katika kipindi kigumu kwani bado alikuwa ni mchanga kwenye taaluma,nilimfariji na kumwambia asikate tamaa na nikammwambia msaada nitakaompa ni wakumtafutia chombo kingine cha habari ambapo nilimtaka aende kwenye Gazeti la Tanzania Daima,aonane na mhariri wa Michezo wa gazeti hilo enzi hizo alikuwa Erick Antony na kabla hajakwenda kumuona mimi nilimpigia simu kaka Erick Antony na kumwomba amsaidie mdogo wangu huyo apate nafasi hapo ya kuandika na Erick alikubali na kuniambia nimruhusu Agnes aje ofisini kwakwe kumuona nikamjulisha Agnes aende kumuona Erick ambaye kwasasa ni Mhariri wa gazeti la Serikali la Habari Leo, alipokwenda kumuona alimkubalia aanze kazi na Agnes alikuja kunishukuru kwa msaaada huo niliyompatia,na kweli akiwa Tanzania Daima ,Agnes ndipo alipoanza kuchomoza kwenye fani ya Uandishi wa habari hapa nchini.Lakini kumbe wakati nampatia msaada huo Agnes naminilikuwa najiandalia mtu wa kuja kunipokea kikazi.Ilipfika mwaka 2006 nilipunguzwa kazi pale gazeti la Tanzania Daima, na niliamua kumpigia simu aliyekuwa Mhariri mkuu wa Gazeti la Tanzania Daima, Deodatus Balile kumuomba aniruhusu nije kufanyakazi katika gazeti analoliongoza, Balile alinikubalia na ilipofika mwaka 2007 ,chini ya uongozi wa Mhariri Mtendaji wa Gazeti la Tanzania Daima,Absalom KIndanda nilipata ajira hadi sasa, ila Agnes alionekana kukata tamaa baadaye akaamua kuacha kazi ya uandishi na kuamua kufanyakazi ya kutafuta matangazo katika gazeti hili,kazi ambayo alikuwa akiifanya hadi anafikwa na mauti.Agnes ,kaka yako Samwel anakulilia,mimi na wafanyakazi wenzako pamoja na ndugu zako tunakulilia na kipenzi chako Kibanda ambaye katika kipindi chote cha kuugua kwako hukupenda kuwasiliana na sisi wote isipokuwa Kibanda na Betty Kangonga wanakulilia.
    Tulikupenda ila Mungu amekupenda zaidi.Hakika Nitakukumbuka mdogo wangu Agnes,nilijitahidi kadri ya uwezo wangu kuakikisha wamadaktari wanaokoa maisha yako lakini kume mungu alikuwa na mipango yake ya kukuchukua.Nakulilia Agnes Yamo.

1 comment:

  1. Hivi? Wasemaji wa "sisi tumekupenda lakini Mungu amekupenda zaidi" kweli hawamaanishi (ingawa sio kwa makusudi) kuwa Mungu ni muuaji? Sidhani kuwa Mungu, kwa wakati wowote anatuondoa huku duniani. Yeye anatupokea tu pale tunapomuendea kwa wakati wetu.

    ReplyDelete

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!