15 November 2014

Huyu ndie mhitimu bora wa chuo kikuu cha UDSM mwaka 2014,anaitwa Doreen Kabuche ana miaka (22) alitangazwa kuwa kinara wa ufaulu kwa kupata alama 'A' 32 na B+ 6 kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima(Actuarial Science)

Kwa alama hizo Doreen Kabuche alipata wastani wa alama Za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu wa alama 5.

Doreen alimaliza elimu yake ya sekondari mwaka 2008 katika shule ya forodhani na alifanikiwa kupata division one  ya point 9,akachaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya  Benjamini Mkapa

Akichukua mchepuo wa EGM  na ndiye aliyekuwa msichana wa kwanza kitaifa kwenye mtihani wa necta kidato cha sita kwa kupata div one ya point 4. 

Hongera sana Doreen wewe ni mfano wa kuigwa


Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!