16 June 2014Watu wanaoshukiwa kuwa wapiganaji wa Al Shabaab wameshambulia kituo cha polisi na hoteli mjini Mpeketoni, pwani ya Kenya .
Makabiliano makali yameripotiwa sehemu kubwa ya Jumapili usiku huku wakaazi wakitorokea msituni karibu na kisiwa cha Lamu.
Shirika la msalaba mwekundu linasema kuwa hadi kufikia sasa watu 48 wanahofiwa kuuawa katika shambulizi hilo lililotokea usiku wa kuamkia leo.
Hata hivyo vyombo vya habari vinasema idadi hiyo huenda ikawa juu zaidi.
Shambulizi lilifanyika usiku wa kuamkia leo pale ambapo watu waliokuwa wamejifunika nyuso zao wakiwa wamejihami vikali walivamia vituo vya polisi , hoteli na benki.
Shambulizi hilo linakuja siku kadhaa baada ya serikali ya Uingereza kufunga ofisi zake mjini Mombasa kwa hofu ya usalama.

 
Duru za jeshi la Kenya zimearifu kuwa wapiganaji hao hawajajitambulisha ni wa kundi gani.
Kituo kimoja cha polisi kilichoshambuliwa na wapiganaji hao Baadhi ya walioshuhudia wamearifu BBC kuwa wameona maiti kadhaa na majeruhi wengi japo Polisi hawajathibitisha ni watu wangapi wameuawa.
 

Kenya imekumbwa na mashambulio kadhaa kutoka kwa wapiganaji wa kisomali wa Al Shabaab tangu ipeleke wanajeshi wake ndani ya Somalia mwaka wa 2011.
Duru kutoka kisiwa cha Lamu zimearifu kuwa wapiganaji hao walifika katika malori mawili na kurusha kifaa kama bomu ndani ya kituo cha polisi kisha wakakivamia na kuiba silaha.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!