17 November 2014

  • Bwana Harusi Amwacha bibi Harusi Kwenye Sherehe ya harusi yao baada ya kuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha aliwataka wapozi kwa ajili ya picha
  • Harusi hiyo iliyofanyika Magharibi mwa mji wa Madinah.
  • Maharusi hawakuwahi kukutana uso kwa uso kabla ya sherehe ya Harusi
  • Wewe si yule msichana ambaye nilikuwa nikimfikiria... sina budi nikuache'
  • Mwanamke mwingine uko uko Saudia amepewa talaka kwa kutojibu mesei ya whatsaApp alotumiwa na mumewe.
Bwana Harusi Amwacha bibi Harusi Kwenye Sherehe ya harusi yao baada ya kuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha aliwataka wapozi kwa ajili ya picha.

Mwnamume wa Kisaudia amemweleza Bi Harusi kuwa amempa talaka Mke wake mpya siku ya harusi yao, baada ya kuona uso wake kwa mara ya kwanza wakati mpiga picha alipowataka wapozi kwa ajili ya picha.

Harusi hiyo iliyofanyika Magharibi mwa mji wa Madinah. Iliingia kitimu timu baada ya bwana harusi kuona uso wa Bi harusi na kutamka hayo aliyoyatamka.

Maharusi hao hawakuwahi kukutana uso kwa uso kabla ya sherehe hiyo wala kuona picha za kila mmoja wao.

Kizaa zaa kilianza pale tu, Bi Harusi aliponyayua veli lake uku akitabasamu kwa dhumuni la kupiga picha za ukumbusho, ndipo bwana Harusi hakaruka kimanga na kutamka kwa hasira uku akisema kwa sauti kubwa '...Wewe si yule msichana ambaye nilikuwa nikimfikiria. Utanisamehe, Nasikitika ila sina budi nikuache... Nimekuacha'
Hivi karibuni kuna mwanamke mwingine uko uko Saudia ambaye amepewa talaka kwa sababu tu, akuweza kujibu mesei ya whatsaApp alotumiwa na mumewe.
Baada ya kuondoa veri uku akitabasamu kwa ajili ya kamera, mume haliruka na kusimama ghafla kwa miguu yake uku akisema kwa hasira, ...Wewe si yule msichana ambaye nilikuwa nikimfikiria. Utanisamehe, Nasikitika ila sina budi nikuache... Nimekuacha'

Kwa mujibu wa gazeti la Daily Okaz, bi harusi ghafla naye aliangua kilio cha machozi kwa mshituko alioupata na kuzimia. Jitihada za ndugu na jamaa hazikuweza kutatua wala kusuruhisha tatizo lililojitokeza.

'Bwana harusi alisema hakuwahi kuona uso bi harusi kabla ya ndoa'

Furaha ya harusi kwa ndugu, jamaa na marafiki iliingia doa na kugubwikwa na machozi ya uzuni badala ya vicheko, nderemo na vifijo 'Wakati bi harusi alipo tamkiwa tu kuwa ameachwa kwa sababu sura yake haikumvutia bwana harusi. Na ndipo bi harusi alipo anguka na kupoteza fahamu.

Mmoja wa waandishi katika mitandao ya kijamii  aliandika kuwa, Bwana harusi amefanya jambo baya na lisilo kubalika katika jamii: 'Amemsababishia mwenzake maumivu makubwa maishani mwake kwa kuwa tu na mtizamo wa kibinafsi na uchoyo wa nafsi, akifikiria kuwa uzuri wa mwanamke ni sura na si tabia.

'Kwa bahati mbaya, vijana wengi wa sasa wanacho angalia wao ni uzuri wa nje au umbo la mwanamke na si tabia wala maadili.

'May God give her a better husband who will appreciate her for who and what she is.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!