21 October 2014


Wananchi kadhaa nchini Ireland, wamejitokeza kwa maelfu kwenye maandamano kupinga ulipaji wa maji.

Pamoja na kuzingirwa na Polisi na wakisaidiwa na helikopta, mamia ya maelfu ya watu kutoka kila pembe ya nchi waliandamana kupinga ulipaji wa bili za maji na maji taka.

"Liwalo na liwe, wengi walisikika wakipaza sauti zao kwa kishindo," alisema Clare Daly. "Tupo hapa kwa maelfu na kwa umoja wetu tunasema kuwa maji ni haki ya msingi kwa binadamu, na si kulipia kulingana na uwezo au matumizi au kulingana na haja ya kila raiya."

Wakionyesha mabango yaliondikwa "Hatuto Lipa" na mengine yameandikwa "Kodi ya Maji ni ukandamizaji kwa wenye majumba." 

Waandamaji walioko mji mkuu wa Ireland, Dublin walitumia zaidi ya saa tatu kuandamana kuzunguka kituo cha ulipaji maji, uku wakipaza sauti zao wakisemaa: "Kenny ndani ya ofisi yako, sikia hii ndio inaitwa nguvu ya Umma!"

Serikali ya Ireland kupitia Bunge lake, lilitangaza kuanzia Mwishoni mwa mwezi wa October kuwa nyumba zote zinapaswa kulipia matumizi ya maji kulingana na matumizi yao. 


Japokuwa serikali imetoa ahadi kuwa, itawasaidia raiya zake kulipia sehemu ya bili za maji mpaka kufikia euro €100 kwa kila nyumba, lakini raiya wameona kuwa mpango huo ni kama danganya toto na wanataka bili zote za maji zisiwepo au kama zitakuwepo basi walipe kwa viwango sawa kwa mwezi na viwe vya chini sana.

Bei ya bili za maji imepangwa kuwa ni (euro) €4.88 kwa lita 1,000 kwa kila nyumba, na kiwango cha lita 30,000 za maji kitagaiwa bure pamoja na nyongeza ya lita 21,000 kwa kila mtoto anayeishi katika nyumba kwa mwaka.

Kulingana na Tume ya mahesabu Nishati Kanuni, Dr McDonnell alisema kaya na watu wazima wanaoishi peke yao watalipa euro € 176. Na kwa ziada ya kila mtu mzima mmoja itakuwa euro € 102 kwa kila mtu mzima wa ziada, malipo ya kawaida ni euro € 278 kwa miezi tisa ya kwanza, hii ni kwa ajili ya malipo kwa kutumia huduma ya maji na maji taka.

Alisema matarajio ya mpaka euro € 1,000 hayata wezekana kwa sababu hakuna nyumba yenye kuishi watu wazima zaidi ya watano.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!