13 April 2014

Inna lillahi wa inna ilayhi raji'un
Sisi sote ni wa MwenyeziMungu, na kwake sisi sote tutarejea

Habari tulizozipata jioni hii, zinaeleza kuwa Mwanamuziki wa siku nyingi na mkongwe wa Muziki wa Dansi nchini, Maalim Muhidin Gurumo (73) aliyekuwa akiimba kwenye Bendi ya Msondo Ngoma ‘Baba ya Muziki’ kabla ya kustaafu mwaka jana, amefariki dunia katika Hospitali ya Taifa Muhimbili alipokuwa amelazwa.

Mzee Gurumo alikuwa anasumbuliwa na maradhi ya Moyo, taratibu za mazishi bado hajizafahamika.

Maalim Muhidin Gurumo alizaliwa uko Masaki, Wilaya ya Kisarawe, Mkoa wa Pwani, mwaka 1941 Na akapata elimu yake ya Msingi Shule ya Pugu kuanzia darasa la kwanza mpaka la tatu.

Mwaka 1956 alichukuliwa na mjomba wake na kuhamia Mkoani Dar es Salaam ambako alisoma madrasa iliyokuwa mtaa wa Lindi, Ilala.

Alisoma elimu ya dini ya Kislam na kuhifadhi Qur'an mpaka mwaka1960 alipojiunga na Bendi ya Nuta Jazz Mwaka 1967 na mwaka huo huo alifunga ndoa na kubahatika kupata watoto wanne.

Bendi ya Nuta baadaye ilibadili jina na kuitwa Juwata, baadaye Ottu Jazz. Mwaka 1978 alihamia Mlimani Park Orchestra na mwaka 1985 alijiunga na Bendi ya Orchestra Safari Sound (OSS- Ndekule).

Mwaka 1990 Gurumo pamoja na mwimbaji Hassan Rehan Bitchuka walirudi Msondo na tangu hapo mwimbaji huyo hajaihama bendi hiyo mpaka anaposumbuliwa na maradhi ya moyo yaliyosababisha kifo chake 13 April 2014
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!