1 September 2014Sindelfingen Ujerumani:  

Mwanamuziki wa nyimbo za Bongo flavour Nasib Abdul (a.k.a Diamond Platnumz) ameponea chupuchupu kula mkong’oto kutoka kwa washabiki wake waliokuwa wakimngojea katika ukumbi uko jijini Sindelfingen Ujerumani.

Fujo zilisababishwa na mwanamuziki huyo kuchelewa kuja kwenye jukwaa, tofauti na ilivyotarajiwa. Onyesho lilitarajiwa kuanza saa nne usiku lakini kitu cha kustaajabisha mwanamuziki huyo aliletwa ukumbini saa kumi za alfajiri, akiwa na promota wake raia wa Nigeria anayeitwa Britts Event.

Washabiki wasio pungua 500 walikuwepo ukumbini siku ya Jumamosi kuamkia Jumapili wakisubiri burudani kutoka kwa mwanamuziki huyo, kitu ambacho hawakukipata, baada ya kuzuka taflani na sinto fahamu ya washabiki. Hasira za mashabiki ziliporipuka baada ya kuona kuwa hata vyombo vilivyofungwa havikuwa ni vyombo vizuri, maana mziki ulikuwa mbovu, licha ya kulipa yuro €25

Polisi wapatao 36 walifika kutuliza ghasia hizo kiasi ilibidi watumie pepper spray ili kuwatuliza washabiki waliokuwa na hasira.  Polisi nchini Ujerumani wanamesema tukio la aibu kama ilo halijawahi kutokea.

Vyombo vya mziki, Viti, meza na Samani zingine zilivunja na kupelekea hasara kubwa kwa mwenye ukumbi.

Watu wapatao nane walijeruhiwa, mmojawapo akiwa mahututi kiasi cha kulazwa katika wodi ya  wagonjwa mahututi (ICU).

Mwimbaji huyo alilazimishwa kuondoka uku akiwa chini ya ulinzi wa polisi kwa usalama wake. Na Mwandaaji raiya wa Nigeria hajulikani alipo mpaka sasa.

Source: stuttgarter
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!