2 June 2012





Wema na Nasib (diamond)enzi za penzi la shatashata, ambalo sasa limebaki historia

MWANAMUZIKI nyota
Tanzania, Diamond amesema kwamba kufanya kwake vizuri katika mahojiano
ya lugha ya kiingereza aliyoyafanya  kwenye jumba la Big Brother hivi karibuni, nchini
Afrika Kusini, ni kutokana na mafunzo mazuri ya kuzungumza lugha hiyo,
aliyopewa na mpenzi wake wa zamani, Wema Sepetu.


Diamond ameyasema
hayo katika kipindi cha XXL cha Clouds Radio- baada ya
kuulizwa siri ya kujiamini kwake kuzungumza vema Kiingereza bila kitete
alipokuwa akihojiwa BBA.


amesema anamshukuru mama yake mzazi na mpenzi wake wa zamani
"Namshukuru sana
mama yangu mzazi kwa kunisomesha, lakini pia namshukuru Wema Sepetu kwa kweli alinisaidia sana wakati nipo naye kunifundisha
kuzungumza Kiingereza kwa kujiamini,"alisema Diamond.


Diamond anakuwa
msanii wa pili kuzungumza hadharani kunufaika na lugha ya Kiingereza
kutoka kwa Wema, baada ya marehemu Steven Kanumba naye kuwahi kusema
hapo awali, alisaidiwa mno na Miss Tanzania huyo wa mwaka 2006 kunyoosha
lugha huyo.
Kwa hisani ya Bongostarz.blog/this day magazine
Kutoka tmark-turn hakika Wema wewe ni mwema kama jina lako lilivyo na pia ni mke mwema isipokuwa huna bahati na hawa watu wanaoitwa wanaume,inshallah mwenyezimungu atakujalia mume mwenye kheri na wewe. 
Categories:

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!