18 August 2014Anaitwa Sewa Haji Paroo alifika Zanzibar akitokea katika wilaya Kutch katika jimbo la Gujarat, nchini India. Mnamo mwaka 1852 alifungua duka la bidhaa mbalimbali huko Zanzibar. Mnamo mwaka 1860 akafungua duka lingine kubwa mjini Bagamoyo na kuweka makazi yake uko.

Biashara zake zikawa kubwa na kuwa tajiri mkubwa sana, alisaidia watu wote bila kujali rangi, dini wala kabila zao. Alinunua majengo mengi na kuyafanya maeneo ya watu wasiojiweza, alijengaja mashule na hospitali kadhaa, katika mji wa mzizima (leo inaitwa Dar ES Salaam). Alijenga hospitali na Kuiita Sewa Haji, ikitoa huduma bure.

Mnamo february 1897 Sheikh Sewa Haji Paroo alifariki dunia, ilikuwa ni huzuni na simanzi kwa wakazi wa Bagamoyo na Mzizima kwa kuondokewa na Sheikh Sewa Haji, maana aliependwa sana na wananchi.

Baada ya kifo chake wakoloni baadaye wakabadilisha jina kutoka Sewa Haji Hospital na kuiita Princess Magreth Hospital, na mnamo 1963 iliitwa ikabadilishwa tena jina na kuitwa Muhimbili Hospital, na wakaipa mojawapo za wodi jina lake Wodi ya Sewa Haji.

MwenyeziMungu Amlipe kila la Kheri Shekhe Sewa Haji, kwa kila jambo la kheri alilolifanya na amsamehe makosa yake.
Aamiyn
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!