Raheem
Raheem
“Kuna vijana wengi kitaani wana ndoto za kufikia hapa nilipo kwenye media but kupata mchongo inakua ngumu so kwa kushirikiana na team yangu ya production “Farasi Entertainment” chini ya director Pete, tumeunda team ya kutengeneza vipindi vya TV na matangazo ya kibiashara ili kutoa nafasi kwa undergrounds kuweza kutoka. Pia Nina recording studio kwa ajili ya Audio ambayo ishaanza kufanya kazi… Kazi ya kwanza kutoka chini ya label “SWAHILI NATION” ni TV show ambayo naifanya mwenyewe ipo tayari na baada ya kupata vipaji vipya kazi zingine zitatoka.. Nikiwa kama kijana niliona fursa na pia NIMETHUBUTU kufanya kitu kikubwa kama hichi ambapo pia kitaweza kutoa ajira kwa vijana wenzangu.”
Raheem amesema wasanii watakaoupamba uzinduzi wa brand hiyo ni pamoja na KING CRAZY GK, NCHA KALI, COUNTRY BOY, DOGO JANJA, M RAP, CLIFF MITINDO, BABYMADAHA na GELLY WA RHYMES.
“Nawaomba wadau wajitokeze kwa wingi ili kuweza kufanikisha mpango huu productive kwenye jamii yetu na pia sponsors tunahitaji support kwenu ili project hii iweze kufanikiwa kwa mwaka 2014,” amesema Raheem.
Unaweza kuwasiliana na Raheem kwa email: raheemprincy@gmail.com.
Stori hisani:bongo5