13 October 2012

 Anakwenda kwa jina la   EUGENE FABIAN Mbio za kulisaka taji la Miss Tanzania amezianzia Mkoani Mara na baade kutwaa taji la Kanda ya Ziwa na anavalia namba 21 kambi ya taifa.
****
WAREMBO 30 wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012 kesho Oktoba 13, 2012 wanataraji kupandaa katika jukwaa la Naura Spring Hotel jijini Arusha kuwania taji la Top Model ambapo mshindi atapata tiketi ya kuingia nusu fainali ya Mashindano ya Miss Tanzania mwaka huu.

Shindano hilo la aijna yake na lililopewa uzito kama fainali zenyewe linaandaliwana Wandago Investment, litafanyikja huku wabunifu mbalimbali wa mavazi wakionesha mavazi yao kupitia warembo wa Miss Tanzania.

Kwa mujibu wa Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye ametaja wabunifu hao ni Noel kutoka Dar es Salaam na Beate Allard na Marlies Gabriel kutoka Arusha.

Jumla ya warembo 30 wanaowania taji la Redds Miss Tanzania 2012, wapo katika ziara ya kutembelea vivutio vya Utalii Kanda ya Kaskazini katika mikoa ya Arusha, Moshi na Manyara.

Mshindi wa shindano hilo la Top Model ataingia moja kwa moja katika hatua ya nusu fainali ya shindano hilo kubwa la urembo nchini Tanzania ambalo linadhaminiwa na Redds Premium Cold.

Mrembo huyo ataungana na Miss Photogenic 2012, Lucy Stephano na warembo wengine 15 watakao ingia hatua hiyo ya nusu fainali. 

Akizungumza na wanahabari mjini Monduli hii leo, Mkuu wa Itifaki wa Kamati ya Miss Tanzania, Albert Makoye amesema kuwa tayari maandalizi hayo yamefanyika na warembo hao watachuana vikali maana warembo wote wapo katika viwango vya hali ya juu.

Burudani kali inataraji kutoka kwa Msanii Lina wa THT huku ratiba nzima ya shughuli hiyo akiishikilia mcheleshaji Mpoki.

Taji la Top Model linashikiliwa na Mrembo Mwajabu Juma.
 
BABYLOVE KALALA ni Mshiriki na 9 akitokea mkoa wa Kagera, akiwakilisha Kanda ya Ziwa.
 

BRIGITTE ALFRED ni Mshiriki namba 26 akitokea Kitongoji cha Sinza na anawakilisha Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Anaitwa VIRGINIA MOKIRI  ni mshiriki namba. akiwakitokea Chuo Kikuu cha DodoUDOM) na akiwakia Elimu ya Juu.
ANANDE RAPHAEL ni mshiriki namba 11 akitokea Mkoa wa Kilimanjaro akiwakilisha Kanda ya Kaskazini.

 
CAREN  ELIAS mshiriki 23 anatokea Mbeya anawakilisha Nyanda za Juu Kusini
 
CATHERINE MASUMBIGANA ni mshiriki na 15 akitokea Kitongoji cha Chang'ombe anawakilisha kanda uya Temeke jijini Dar es Salaam.
 
DIANA HUSSEIN amepata namba ya ushirtiki 20, akitokea kitongoji cha Dar Indian Ocean, akiiwakilisha Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
  
FINA REVOCATUS anavaa namba 12 akitoka Chuo cha Usimamizi wa Fedha IFM, akiwakilisha Kanda ya Vyuo Vya Elimu ya Juu.
BELINDA MBOGO  ni mshiriki na 29 akitoka mkoa wa Dodoma akiwaklilisha Kanda ya Kati
 
EDDA SYLVESTER amepata namba 22, akitoka Kigamboni na anaiwakilisha Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam.
 
ELIZABETH DIAMOND anavalia namba 2 akitokea mkoa wa singida, akiwakilisha kanda ya Kati.
 
FATMA RAMADHANI nambari yake 25 akitoka chuo cha Uandishi wa habari Arusha ASJ, anawakilisha Kanda ya Elimu ya Juu.
FLAVIAN MAEDA anavalia namba 10 akitokea kitongoji cha Kurasini mwakilishi wa kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Kutoka Kahama- Shinyanga ni HAPPINESS RWEYEMAMU ananamba 8 anawakilisha Kanda ya Ziwa.
Huyu ni HAPPYNESS DANIEL namba yake ya ushiriki ni 19 anatokea jiji la Mwanza akiwakilisha Kanda ya Ziwa.
IRINE VEDA anatokea Lindi na kupata namba 16 akiuwakilisha Kanda ya Mashariki
JESCA HAULE ni mshiriki namba 14, akitoka kitongoji cha Chang'ombe anawakilisha Kanda ya Temeke jijini Dar es Salaam.
Anatoka Mji kasoro Bahari-Morogoro ni JOYCE BALUHI akiwa ni mshiriki 13 anawakilisha Kanda ya Mashariki.
JOYCE BALUHI ni mshiriki 13 akitokea kitongoji cha Dar Indian Ocean, akiiwakilisha Kanda ya Kinondoni jijini Dar es Salaam.
Huyu ni LIGHTNESS MICHAEL anavalia 5, akitokea Dodoma akiwakilisha Kanda ya Kati.
Kutoka mkoa wa Manyara ni LUCY STEPHANO mshiriki namba 4 akiwakilisha Kanda ya Kaskazini.
MAGDALENA ROY mshiriki namba 6, kutoka Kitongoji cha Dar City Centre akiwakilisha Kanda ya Ilala.
Anaitwa Mary Chizi akitokea kitongoji cha Ukonga, anavalia namba 17, akiwakilisha Kanda ya Ilala jijini Dar es Salaam.
Yeye ni MAGDALENA ROY mshiriki nambari 18, kutyoka mkoa wa Iringa akiwakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini.
Jinalake ni NOELA MICHAEL yupo na namba 27, anashikilia taji la kitongoji cha Tabata na ni mwakilishi tegemeo wa Kanda ya Ilala.
Rose Lucas ana namba 28 akitokea Mkoa wa Pwani akiwakilisha Kanda ya Mashariki
VENCY EDWARD  ni mshiriki nambari 7, akitoka Mkoa wa Rukwa akiwakilisha Kanda ya Nyanda za Juu Kusini
WARID FRANK huyu ni mshiriki namba 30 akitokea Arusha ana kuiwakilisha  Kanda ya Kaskazini.
Anaitwa ZUWENA NASIB akiwa ni mwakilishi pekee wa chuo Kikuu Huria OUT.

Endelea kutembelea Father Kidevu Blog na ukurasa wa 
http://facebook.com/ReddsMissTanzania2012
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!