27 May 2015


Taarifa zilizo tufikia ni kwamba, Muigizaji Maarufu wa Radio na Television, Bi Catherine Mapunda, Maarufu kwa Jina la Uigizaji Bi Nyakomba, amefariki dunia.

Marehemu Bi Nyakomba alipata umaarufu katika michezo ya maigizo redioni wakati huo ikirushwa na Redio Tanzania (RTD) akishirikiana na wasanii wenzake wakiwemo Hamisi Tajiri al maarufu Meneja, Ibrahim Raha al maarufu Mzee Jongo, Bakari Mbelemba al maarufu Mzee Jangala, Mzee Kagunga, Mzee Majengo na wengine,


Amefariki katika hospitali ya Jeshi la Polisi katika barabara ya Kilwa, alikopelekwa usiku wa kuamkia tarehe 25 May 2015 baada ya kuzidiwa.

Bi Nyakomba alikuwa akisumbuliwa na ugonjwa wa kisukari tangia mwaka 2012.

Marehemu Bi Nyakomba amezikwa tarehe 26 May 2015 saa tisa alasiri kwenye makaburi ya Chang'ombe jijini Dar es Salaam baada ya ibada ya mazishi iliyofanyika katika Kanisa Katoliki la Mtakatifu Maurus, Kurasini.

Ndugu wa familia ya marehemu wamesema Bi Nyakomba amefariki akiwa na umri wa miaka 64 akiacha watoto sita na wajukuu kumi na watatu.Enzi za uhai wake, Channel TEN iliwahi kufika katika nyumba yake huko Keko Juu katika Kata ya Mburahati, Manispaa ya Temeke ili kumjulia hali wakati akiugua pamoja na mambo mengine, alihusia wasanii hususan vijana kote nchini, kuifanya sanaa kwa nidhamu kwa kuwa ni kazi rasmi kama kazi nyinginezo.

Blog ya tmark-turn inawapa pole na mkono wa rambirambi kwa ndugu, jamaa, marafiki na Watanzania wote na wapenda sanaa kwa ujumla.0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!