17 July 2015


Assalamu Alaikum Wa Rahmatu Allah Wa Barakatuh

'Iydul-Fitwr Al-Mubaarak
Taqabbala Allaahu Minnaa wa Minkum


Kwa Munaasabah huu wa furaha wa siku hii tukufu ya ‘Iyd Al-Fitwr tunapenda kuchukua fursa hii kuwawasilishia salaam zetu za siku hii na du'aa njema kwenu wote, tukimuomba Allah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutaqabalie 'amali zetu na zenu ‘TAQABBALA ALLAAHU MINNAA WA MINKUM’ (Hivi ndivyo Maswahaba watukufu walivyokuwa wakiambiana pindi wanapokutana katika siku ya 'Iyd). Na tunamuomba Yeye Aliyetukuka na Mweza, Awajaalie furaha, amani, mapenzi, siha na Iymaan pamoja na karama na utukufu katika masiku yote ya uhai wetu.

Mwisho, bila kuwasahau wenzetu katika du'aa zetu leo na kila siku. Ndugu zetu Waislam waliopo palipokuwa Qiblah cha kwanza cha Uislam, na Msikiti wa tatu kwa utukufu na hadhi, Palestina hasa walioko Gaza. Na wengineo walio katika dhiki za ukandamizwaji, vita, njaa na machafuko popote walipo Waislamu ulimwenguni.
Tunamuomba Allah (Subhaanahu Wa Ta'ala) Atutakabalie du'aa zetu na za Waislam wote duniani, Aamiyn

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!