Huyu ndie mhitimu bora wa chuo kikuu cha UDSM mwaka 2014,anaitwa Doreen Kabuche ana miaka (22) alitangazwa kuwa kinara wa ufaulu kwa kupata alama 'A' 32 na B+ 6 kati ya masomo 38 ya shahada ya Takwimu Bima(Actuarial Science)
Kwa alama hizo Doreen Kabuche alipata wastani wa alama Za ufaulu (GPA) 4.8 na kuacha alama 0.2 ili kufikia kiwango cha juu kabisa cha ufaulu wa alama 5.
Doreen alimaliza elimu yake ya sekondari mwaka 2008 katika shule ya forodhani na alifanikiwa kupata division one ya point 9,akachaguliwa kujiunga na shule ya sekondari ya Benjamini Mkapa
Akichukua mchepuo wa EGM na ndiye aliyekuwa msichana wa kwanza kitaifa kwenye mtihani wa necta kidato cha sita kwa kupata div one ya point 4.
Hongera sana Doreen wewe ni mfano wa kuigwa
0 comments:
Post a Comment