20 August 2014


Mwanamume mmoja mkazi wa Saudia, ametoa kali ya mwaka pale alipotimua mbio kiasi cha kuwashangaza watu wa usalama wa kiwanja cha ndege katika moja viwanja vya ndege nchini Saudia.

Mwanamume huyo mwenye asili ya Misri alikubali kumuoa mwanamke kutoka nchini kwao Misri, baada ya kuonyeshwa picha yake na kaka yake.

Bwana harusi aliwasili kiwanja cha ndege mapema uku akiwa na hamu na bashasha tele na tabasamu kubwa akimsubiri bibi harusi kwa saa kadhaa, kabla ya ndege iliyomleta bibi harusi kuwasili kiwanjani.

Mwandishi wa Gazeti la Kiarabu la nchini Misri Al Watan litokalo kila siku, amenukiliwa akiripoti kuwa...
"Baada ya bwana harusi kutambulishwa na kumuona bibi harusi, ghafla alitimua mbio kama mtu aliyeona mzuka au kitu cha kutisha.

Kiasi cha kuwafanya walinzi na watu wa usalama wa kiwanja cha ndege kumkimbiza wakidhania kuwa ameiba kitu."

Gazeti ili limenukuliwa bila kutaja majina ya wahusika wala kiwanja cha ndege, lilipotokea ilo tukio.

Baada ya wana usalama wa kiwanja cha ndege kumkamata bwana harusi, walimuhoji kilichomfanya mpaka kutimua mbio kiasi kile, naye alinukuliwa akisema kuwa. "Alishtushwa na mwonekano wa bi harusi na hataki tena kuwa pamoja naye wala kuishi naye kama mume na mke."

Bibi Harusi aliomba talaka kisheria pamoja na fidia kwa kupotezewa muda wake.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!