Kuna siku moja nilikuwa naangalia kipindi katika Luninga (TV), walikuwa wakionyesha maisha ya wadudu mbalimbali. Mojawapo ya wadudu niliovutiwa nao ni Nyuki na wadudu wengine wa jamii ya Chungu (Ants).
Kwa kweli nilivutiwa sana na maisha ya hawa viumbe wadogo ambao katika maisha yetu hatuwapi nafasi hata ya kuwatafakari japo kwa sekunde chache tu. Ni mpaka pale tunapowaona kuwa ni kero ndio tunashtuka kuwa wapo.
Wadudu awa kwa kweli naweza kusema kuwa ni wadudu wenye uwezo mkubwa katika kukabiliana na maisha yao ya kila siku. Jambo moja niliovutiwa nalo ni jinsi ya mpangilio wa maisha yao katika mashimo yao na vichuguu vyao.
Kwanza kila mkazi wake anafata amri bila ya kusita. Jambo ili linastaajabisha kidogo, naanza ujiuliza nini siri yake. Muda nagundua kuwa, vichuguu hivi vya mchwa na hata makazi ya nyuki vimejengwa katika hali ambayo inampa nafasi kila mkazi, kufanya kazi zake bila tatizo lolote na bila usumbufu wa hali yoyote.
Kamera ya mchukuwaji wa hii picha naye anastahili sifa na ujasiri na uvumilivu kwa kweli, mchukuwaji wa picha ametuonyesha vyumba mbalimbali kwa kazi tofauti tofauti mfano, Maghala ya chakula ni makubwa na kila mchwa inakuwa ni rahisi kwake kufika hapo bila ya usumbufu wowote. Kuna vyumba kwa ajili ya kutotolea mchwa wapya na kuna sehemu maalum kwa ajili ya mawindo mapya na kile ambacho hakina faida au hawakiitaji basi wanakitoa nje kabisa ya kichuguu chao na kukitupa mbali.
Kwa kweli mambo nilio ona ni mengi lakini lengo langu si kuzungumzia maisha ya wadudu awa, japokuwa kuna mengi ya kujfunza kutoka kwao. lengo langu haswa ni kuangalia maisha yetu majumbani mwetu na jnsi tunavyoishi na kukusanya kila chenye uwezekano wa kukusanywa na kuwekwa kwenye majumba yetu.
Hebu angalia kwenye majumba yetu tunamoishi, na jinsi upangaji wa vitu mbalimbali ndani ya nyumba, yaani tuna shindwa na hata na wadudu katika mipangilio. Utakuta mtu kanunua fenicha mpya, lakini zile za zamani ambazo ukizionea aibu na ukutaka hata kuwakaribisha rafiki zako kuja nyumbani kwako, bado unazitafutia nafasi humo humo ndani. Kuzitupa au kuzigawa unaona tabu au siju unaona hasara, hakuna anayejuwa kwa kweli.
Utakuta nguo ambazo hazikutoshi tena, kuna zingine ulipewa zawadi ulipomaliza kidato cha nne ili ukatokezee kwenye mahafari ya shule miaka kumi kama si ishirini iliyopita, bado unazo, nguo haikutoshi tena, maana ushaongezeka toka kiuno nchi 28 mpaka sasa unavaa kiuno nchi 42, bado unayo tu, ukiulizwa eti kumbukumbu kutoka kwa mjomba wako.
Ukiingia uko kunakoitwa stoo, ni mazalia ya panya, mende na wadudu wengine wanaoishi bila ya kulipa kodi ya nyumba. Magodoro tangia ukisoma boarding school, na lile uliloanzia maisha ulipomaliza JKT ukahama nalo, bado unalo tu, japokuwa sasa ni mtu na familia yako na umekwisha nunua magodoro mapya, lakini yale ya zamani zamani badala ya kugawa umeviringisha na kuaweka juu ya kabati, maana kule stoo hakuna nafasi tena. Ukiulizwa unakiri kuwa kweli uvitumii kwa sasa, ila kuna uwezekano siku ukavitumia, lini haijulikani.
Uko kabatini kwako kuna nguo ambazo ulivaa ukiwa secondary mpaka leo bado unazo, ukiulizwa eti ni ukumbusho au utazivaa ukipungua, sasa utapungua lini, ulikuwa ukivaa kiuno 28 mpaka leo una kiuno 42 plus...
Uko jikoni ndio shida iliposhika hatamu! Mivyombo ya plastiki imepaukiana imeyayuka na moto ipo tu eti vyombo vya watoto, maana ukiwanunulia vya udongo awachelewi kuvunja, watakutia hasara.
Hotpot zote zimekata roho maana plastiki za nje zimepeana taraka na sufuria lake la ndani, lakini bado unalo tu. Kila ukibahatika kununu chupa za maji basi utahakikisha chupa zake huzitupi, vidoo vya sadolini, kila mahala hata hazitumiki zipozipo tu, hata maua hazifai kupandia we unazogo tu hutupi, na kuzihitaji wala huzihitaji.
Ukiangalia vyombo vya udongo vina mapengo na magego kama barabara iliyopigwa mabomu, na kila kimoja na dizaini yake havifanani kwa sababu seti zote zimesha vunjika vunjika hivyo ndio vimebakia.
Ukija ndani kwenye hiyo meza ya kuipambia, wenyewe mnaita Dressing table, ni hatari kwa kweli, maana imejaa mikopo na mibox haina hata kazi, perfume ya mwaka 2000 imekwisha malizika, weew kopo/chupa yake unayo tu, ukiuliza eti ukumbusho wa zawadi, ulipewa na nanii wako.
Uko stoo ukiambiwa uingie mwenyewe unaogopa, sababu stoo imekuwa mji wa panya na jamaa zao mende, maana imejaa vitu visivyo hitajika, stoo imekuwa ghetto la panya, maana vilivyokuwemo humo ni vile ambavyo huvihitaji tena, lakini kuvigawa au kuvitupa unaona hasara.
Sasa na lile pale nje nini niin, unaambiwa lile ni gari, unajuliza sasa mbona limebakia sikrepa tu, si uwape wanao kusanya vyuma, wakavipeleke kwa resaiko. Hutaki kisa ni gari la urithi la kutoka kwa baba yake na babu yako. Lipo tu hapo limekuwa makazi ya paka shume na wadudu wengine.
Kutupa vitu visivyo hitajika hamtupi eti Dhambi na kuvigawa haviwezekani tena maana havina hadhi tena ya kupewa mtu, vimekosa ile uhalisi wake, hakuna hanaye vitaka wala kuviulizia.
Ndio maana kila siku hamuishi kupishana mahospiitalini, mara leo kikohozi kesho kifua kizito, mara mafua na flu. Kwanini msiumwe na mnakaa dampo!?
Tumewaambukiza mpaka watoto wadogo, maana wanajuwa kuwa nyumbani kwao hata kikopo cha icecream au kopo la plasitiki la siagi havitupwi vinaoshwa vinawekwa hapo. Halafu bado unaendelea kumuomba Mungu akupe, akupe uweke wapi na kwako pameshajaa au uoni!?
Huu ni ugonjwa? Na wengi tumehathirika na haya maradhi ya kutopenda kutupa au kugawa tusivyo vitumia wenye lugha yao wanaita "hoarder disorder".
0 comments:
Post a Comment