26 June 2013

Inaweza kuonekana kama ni simulizi tu au jambo ambalo si la kweli, lakini kwa wakaazi wa Las Vegas nchini Marekani, wanamtambua na kumfahamu vizuri Bwana Wesley Warren Jnr, mwenye umri wa miaka 49.
Wesley Warren Jnr, amekuwa na tatizo ili kwa miaka isiyopungua minne (4), kitaalam linajulikana kama scrotal lymphedema kwa tafasiri nyepesi twaweza sema ni Busha (Mshipa).


Tatizo la Wesley limechangiwa sana na mfumo mmbovu wa huduma za afya nchini Marekani, mfumo ambao hauwapi nafasi walalahoi kuweza kutibiwa kama hawana pesa au bima ya afya ambayo inaweza kutoshereza matibabu ya maradhi mbalimbali yanayowasumbua wananchi. Wesley alikuwa anatakiwa kulipa kiasi kisicho pungua dola laki moja $100,000. Kiasi ambacho hakuwa na uwezo wa kukipata.

Tatizo la Wesley, lilianza usiku mmoja mwaka 2008 alipojigonga kwenye kingo za kitanda kwa bahati mbaya, na kusababisha maumivu makali kwenye mapumbu yake, na kuanzia siku hiyo pumbu zake zikaanza kuvimba kidogo kidogo mpaka kufikia ukubwa wa kilo zisizopungua 63. 
  
Wesley baada ya kuona hali si nzuri na hapati matibabu yoyote alianzisha kampeni maalum kwenye page facebook na kuomba michango ya wahisani mbalimbali, na kuweza kukusanya dola 2000 na uku akipata pesa kidogo za kujikimu kutoka serikali (social welfare/social security fund). Bahati mbaya zaidi watu wa serikali walipoangalia account yake ya bank na kuona kuwa ana kiasi hicho cha pesa wakaacha kabisa kumpatia pesa za kujikimu, hali hii ikampelekea Wesley kutumia pesa alizokuwa akichangiwa na wahisani kwenye mahitaji ya chakula na matumizi mengine.
Lakini kama tunavyojuwa Mungu amtupi mja wake, Wesley alionekana na madaktari na wakaweza kumsaidia tatizo lake, bila malipo yoyote yale. Operesheni yake ilichukuwa masaa yasiopungua kumi na tatu (13). Na aliweza kuamka kutoka kwenye usingizi mzito wa madaya ya kumlaza baada ya siku mbili.0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!