Kambi Maarufu ya wahamiaji na wakimbizi, mjini Calais, nchini Ufaransa yenye kujulikana kwa jina la THE JUNGLE.
Hii ni Kambi ya Wahamiaji na Wakimbizi iliyopo Mjini Calais, Ufaransa.
Wengi wao ni kutoka Eritrea, Ethiopia, Libya, Afghanistan, Iran, Iraq, Sudan na Syria
"Kila aliyeko kwenye kambi hii mjini Calais si kwamba anapenda au anataka kuishi hapo Calais la hasha. Kila mtu aliyepo hapo ndoto yake ni kwenda kuishi nchini Uingereza."
Takriban watu 4,000 wanaishi katika kambi karibu na bandari ya mji wa Calais. Idadi kubwa ni vijana, lakini pia kuna wanawake wachache na watoto. Wengi wao ni kutoka Eritrea, Ethiopia, Libya, Afghanistan, Iran, Iraq, Sudan na wakimbizi kadhaa wanatoka nchini Syria.
Wote wamesafiri kwa muda wa wiki au miezi kadhaa au hata miaka wakizunguka nchi za Ulaya kwa lengo la kufika Calais, ambayo ipo maili zisizo pungua 30 kutoka mkondo wa bahari ya Waingereza kuelekea Uingereza (English Channel).
Hali ya kambi, si nzuri kabisa kwa binadamu yoyote kuishi humo.
Kambi imezungukwa na dampo, kiasi cha kusababisha matatizo ya kiafya kwa wakazi wake. Magonjwa kama vile ukurutu (Upele) ni jambo la kawaida – magonjwa yamacho na maambukizi ya kuumwa kifua unaosababishwa na vumbi na mchanga.
Na nje ya Kambi kuna uzio ambao una ncha kali na polisi wakipokezana ili kuwazuiya wale wote ambao watajaribu kuingia eneo ambalo magari makubwa yameegeshwa kusubiria zamu ya kuingia kwenye shimo au handaki ambalo linapita chini ya bahari kuanzia Ufaransa mpaka Nchini Uingereza.
Kuna mashirika yasiyopungua matatu na baadhi ya watu binafsi ambao wanajaribu kwa njia moja au nyingine kuwasaidia wahamiaji hao na wakimbizi waliopo hapo kambini.
Mara chache chache ukiwa ni mkaazi wa hapo unaweza kupata hema la kulalia, blanketi na hata vyakula vya kwenye makopo.
Wakazi wengi ambao wamejaribu kuingia Uingereza kwa kuruka uzio wa waya zenye ncha kazi wamejikuta wakijeruiwa aidha na waya zenye ncha kali au kupigwa na polisi wa ufaransa. Wapo ambao wamejikuta wakiumizwa na malori ya mizigo na hata kupoteza maisha.
0 comments:
Post a Comment