27 November 2014


Jeshi la polisi Tanzania limezindua mpango kazi wa miaka mitatu kupambana na unyanyasaji wa kijinsia na unyanyasaji wa watoto katika nchi, gazeti la Daily News la Tanzania liliripoti.

Waziri wa Mambo ya Ndani Emmanuel Nchimbi alitangaza mpango huo wakati wa Siku 16 za kampeni ya Harakati Dhidi ya Unyanyasaji wa Kijinsia, kampeni ya kimataifa inayolenga kuinua uelewa kuhusu suala hili.

Takribani asilimia 45 ya wakina mama wenye umri wa miaka kati ya 15 hadi 49 waliripoti kunyanyaswa kimwili au kijinsia katika maisha yao, kwa mujibu wa Utafiti wa Demografia na Afya nchini Tanzania wa mwaka 2010.

Watoto nao wako katika hatari kubwa, msichana mmoja kati ya watatu na mvulana mmoja kati ya saba wamenyanyaswa kijinsia, na zaidi ya asilimia 70 walinyanyaswa kijinsia kabla ya kufikisha umri wa miaka 18.

"Jeshi la polisi linawajibika kuboresha mwitikio wake kwa manusura wa [ukatili wa kijinsia] na unyanyasaji wa watoto," Inspekta Jenerali wa Polisi Said Mwema alisema.

Wakati huo huo ripota wetu anatuhabarisha kwamba, Serikali ya Tanzania imetoa mafunzo kwa maafisa 300 wa jeshi la polisi nchini kote katika juhudi za kukabiliana na unyanyasaji dhidi wa wanawake na watoto, Naibu Waziri wa Sheria na Masuala ya Katiba, Angellah Kairuki, aliliambia bunge siku ya Jumatano.

Miongoni mwa waliopewa mafunzo ya kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia ni pamoja na maafisa 110 wa polisi, maafisa 110 wa magereza, mahakimu 60, madiwani 80 na pia viongozi wa kimila, kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania.

Kairuki alisema Tume ya Haki za Binaadamu na Utawala Bora na taasisi nyengine pia zimechangia kwenye kujenga mwamko wa kushughulikia kesi za unyanyasaji wa kijinsia, na zimetoa mafunzo kwa maafisa tendaji wa wilaya katika mikoa 18 ya bara na mitano ya Zanzibar.

Kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa tarehe 19 Februari, unyanyasaji wa kijinsia ni mkubwa sana Zanzibar ukiwa na kesi 996 na wa uko chini kabisa katika wilaya za Mara na Singida.

"Baada ya utafiti wa kina, imefahamika kwamba wanawake wengi katika maeneo ya vijijini yaliyo masikini wako kwenye hatari ya uwezekano wa kubakwa na aina nyengine za ghasia za kijinsia," alisema rais wa GG Trust, Stella Mathias. "Mafunzo haya yanakusudiwa kuwapa mbinu bora zaidi dhidi ya wabakaji."

Mathias alisema askari hao wa kike watawafundisha wanawake wengine mafunzo hayo ikiwa ni sehemu ya kampeni kubwa ya kuwafundisha asilimia 80 ya wanawake wa Tanzania namna ya kujilinda dhidi ya ghasia.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!