30 November 2014


Kristina Pimenova mwenye umri wa miaka 9 ndio msichana mrembo kuliko woteduniani (!?) aliyechaguliwa mwaka huu.

Ni msichana mwenye umri wa miaka tisa kweli, na ili jambo limekuwa ndio sababu ya watu kuanza kujadili kama inafaa kuwa na watoto katika mambo ya urembo au la.

Kristina Pimenova mzaliwa wa Urusi, mwenye macho makubwa ya kibuluu ambayo kwa vigezo vya watu wa ulaya ndio macho yanayosemekana kuwa yenye kuvutia sana, ana midomo iliyokaa vema kama upinde na dimples ndogo pembeni mwa midomo yake.


Vitu hivyo pamoja na vigezo vingine ndio vimemfanya Kristina Pimenova mzaliwa wa Urusi kuchaguliwa kuwa binti mrembo kuliko wote. Zingatia kwamba vigezo hivi ni kwa watu wa Ulaya tu.

Kristina Pimenova amekuwa katika ulimwengu wa urembo tangia alipokuwa na miaka mitatu tu. Na amefanyakazi katika makampuni ya kutengeneza manukato kama vile Roberto Cavalli, Dolce & Gabbana na Armani.

Kwenye ukurasa wake wa Facebook, Kristina Pimenova ameandika kuwa anafurahiya sana kazi za urimbwende, hasa catwalk na maonyesho ya mitindo.


Ukweli kwamba kumekuwa na hali ambayo inatishia usalama wake na haswa ukizingatia commets zinazowekwa kwenye ukurasa wake wa facbook, ukurasa ambao una wafuatiliaji wasiopungua milioni mbili.

Wapo washabiki wake wanao muona kama ni msichana mrembo tu na wakimsifia hapa na pale na wakimtakia mafanikio kama msichana mdogo, lakini kuna wale ambao wana comment kwa viashilio vya ngono. Ambazo nyingi zimefutwa.

Comment nyingi ni za wanaume watu wazima wakiandika maneno kama vile "beautiful, I think I'm in love" na "marry me."


Hali kama hii imepelekea wazazi wake kuwa na wasiwasi picha zake zikachukuliwa kutoka kwenye mitandao na kutumika kwenye mitandao ya ngono.

Na vilevile kuna uwezekano wa Kristina kuja kunyanyasika kijinsia kama hatua za kiusalama hazita chukuliwa, na ili si kwake yeye tu, bali wa wasichana na wavulana wadogo wengi wenye kuhusishwa na biashara ya urembo duniani kote.

Je Msomaji una maoni gani kwa watoto wadogo kushirikishwa kwenye biashara ya Urembo na uonyeshaji wa mavazi na matangazo ya Mafuta ya Manukato!?

Reactions:

0 comments:

Post a comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!