27 November 2014


Ghasia zinazotokana na jinsia zimeongezeka katika baadhi ya maeneo ya Zanzibar na zimeendelea kuwa za juu katika maeneo mengi ya Tanzania, kwa mujibu wa ripoti iliyotolewa siku ya Jumatano (tarehe 19 Februari) na Chama cha Waandishi wa Habari Wanawake cha Tanzania (TAMWA).

Katika kukusanya ripoti ya ghasia za kijinsia ya mwaka 2013, waandishi wa habari 30 wa Tanzania walikusanya data baada ya kupata mafunzo ya uandishi wa habari za uchunguzi kutoka kwa Shirika la Idadi ya Watu la Umoja wa Mataifa. Waandishi hao wa habari baadaye waliunda Mtandao wa Waandishi wa Habari dhidi ya Ghasia za Kijinsia.

"Matokeo ya utafiti wa siku kumi uliofanywa na waandishi hawa wa habari yamethibitisha bila shaka kwamba [ghasia za kijinsia] bado ni za kiwango cha juu nchini hii," alisema mjumbe wa bodi ya TAMWA, Gladness Hemed Munuo, katika uzinduzi wa ripoti hiyo jijini Dar es Salaam, kwa mujibu wa gazeti la Daily News la Tanzania.

Ripoti hiyo ilikusanya data za ubakaji, mimba za umri mdogo, ndoa za utotoni, utekelezwaji wa wanawake na watoto, na ghasia za majumbani katika wilaya tano za Zanzibar na 13 za bara, liliripoti gazeti la The Citizen la Tanzania.

Wachunguzi waligundua kwamba kiwango cha matukio kilikuwa cha juu visiwani Zanzibar kukiwa na visa 996, na kiwango kidogo zaidi kilikuwa kwenye wilaya za Mara na Singida. Katika utafiti wa mwisho, asilimia 20 ya wanawake wa Singida waliripoti kubakwa, lakini katika utafiti huu wa karibuni hakukuwa na kisa cha ubakaji kilichoripotiwa.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!