10 September 2014


Hizi ajali kwenye vyombo vya usafiri uko Bongoland, zinaelekea sasa kuwa kama vile ni jambo la kawaida, maana haipiti muda mrefu bila kusikia aidha Meli imezama, Mabasi yamegongana au kupinduka, Daladala imeuwa, Bodaboda zimegongwa, kiasi naanza kujiuliza, Hivi Vyombo vya Usafiri ni kwa ajili ya kuwasafrisha abiria kuelekea kule wanapotaka kwenda au Ni Majeneza Yanayo Tembea au Ni vyombo vya Usafiri vya Kuwapeleka Watu Akhera!?

Kuna mambo mengi ya kujiuliza, kulikoni haya yanatokea kila leo na hakuna hatua madhubuti zinazochukuliwa aidha kupunguza ajali kwenye vyombo vya usafiri au kuwa na mfumo madhubuti wa kuhakiki utaalam wa awa madereva kabla ya kupewa dhamana ya kubeba abiria.

Inapotokea Mabasi ya abiria au malori ya kubeba mizigo, kugongana uso kwa uso, hii inaashiria nini? Kama si uzembe na umakusudi wa madereva kushindwa kuheshimu sheria za barabarani.

Najiuliza tena, hivi kuna vyombo vya kisheria vya kudhibiti na kufatilia vyombo vya abiria vilivyosajiliwa kubeba abiria? Uko mijini tunaweza kusema kuwa kuna askari wa barabarani (Trafic Police) ambao kazi yao kubwa ni kuangalia nidhamu na usalama wa wote wenye kutumia barabara. Inapotokea polisi wa usalama barabarani anapomsimamisha dereva wa Basi la Abiria lililovunja sheria, na badala ya kumwajibisha dereva anachofanya ni kwenda kuongea na Kondakta, ili ni gonjwa kubwa sana (Rushwa) ambalo abiria wanapaswa nao kulikemea waziwazi, kwa maana kila wanapopanda vyombo vya usafiri, basi wawe makini na washiriane kwa pamoja kukemea pale wanapo ona sheria za barabara zinavunjwa na dereva wa basi walilopanda. Labda kidogo inaweza kusaidia kupunguza uzembe unaopelekea ajali ambazo zinaweza kuepukwa.
  • Abiria Mkiwa Kwenye Bus, Msikubali Wala Kumruhusu Dereva Kuchepuka, Hakikishine Anabaki Njia Kuu.
  • Abiria Mkiwa Kwenye Bus, Msikubali Wala Kumruhusu Dereva Mwenye Kuonyesha Dalili Za Ulevi.
  • Abiria Mkiwa Kwenye Bus, Msikubali Wala Kumruhusu Dereva Mwenye Kuendesha Mbio, Nje Ya Mwendo Kasi Uliopangwa.
  • Abiria Mkiwa Kwenye Bus, Msikubali Wala Kumruhusu Dereva, Kuchomekia Ili Haweze Kupata Tripu Nyingi.


Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!