3 August 2013


MCHEZAJI wa zamani wa Coastal Union ya Tanga, Idrisa Ngulungu aliyefariki jana kwa ajali ya gari anatarajiwa kuzikwa leo Mjini morogoro.
Idirisa Ngulungu ambaye alitamba na kikosi cha Costal Union mwishoni mwa miaka ya themanini hadi mwanzoni mwa miaka ya tisini,pia Alikuwepo kwenye kikosi kilichotwaa ubingwa wa Tanzania Bara mwaka 1988.
Kwa mujibu wa kaka wa marehemu, Hussein Ngulungu ambaye nae ni mchezaji wa zamani wa Taifa Stars alisema Idrisa amefariki kwa ajali ya gari iliyotokea eneo la Kisaki mkoani Morogoro.
Hussein Ngulungu alisema kuwa Idrisa na ndugu wengine walikuwa wanaelekea Kisaki kwenye mazishi na kwa bahati mbaya gari walilokuwa wanasafiria lilichomoka tairi la mbele na kusababisha ajali hiyo iliyopoteza maisha ya Idirsa pamoja na ngugu yake mwingine wa kike.
Tmark-turn inawapa pole familia ya marehemu.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!