2 June 2012





SHIRIKISHO  la Ngumi la Kimataifa (IBF) pamoja na Kamisheni ya Ngumi
za Kulipwa Tanzania (TPBC) zinamlilia bingwa wa IBF wa mabara na bingwa
wa dunia wa WBU Magoma Shaban.

Magoma amefariki jana katika hospitali ya Bombo jijini Tanga atakumbukwa kwa umahiri wake kwenye ngumi za kulipwa.

Mwaka 1998 ndio Safari ya Magoma Shaban kwenye ngumi za kulipwa iliponzia katika
uwanja wa Mkwakwani jijini Tanga mwaka.

Ikiwa ndio kwanza Onesmo Ngowi akiwa
ameteuliwa na Rais wa zamani wa IBF Robert Lee Sr toka
Marekani kuanzisha shirikisho hilo la IBF katika bara la Afrika.

Katika uwanja huo Magoma Shaban alipigana na Joseph Waweru toka
Kenya na kumshinda kwa KO na kutangazwa kuwa bingwa wa IBF katika bara
la Afrika uzito wa flyweight.

Mwaka 2000 Magoma chini ya kampuni ya Capital Promoters Limited
inayomilikiwa na mwanahabari bwana Gabriel Nderumaki alipigana
na bondia Totim Lukunim toka Thailand katika ukumbi wa PTA kugombea
mkanda wa IBF wa mabara katika uzito wa Flyweight na kumshinda kwa KO
katika raundi ya 4,na hiyo ndio  ikawa mwanzo wa safari ya Magoma Shaban kwenye 
ulimwengu wa ngumi za kulipwa.

Magoma Shaban alipigania ubingwa wa dunia wa WBU nchini Italy na kumshinda bondia Ferid Ben Jeddou kwa TKO katika raundi ya 6.

Magoma alikuwa ni bondia aliyeing'arisha Tanzania na bara zima la Afrika katika medani ya ngumi za kulipwa duniani.

 IBF  imetangaza rasmi kuuita mkanda wa uzito wa Fly aliokuwa anachezea Magoma kuwa "Mkanda wa Magoma Shaban" katika mapambano yote yatakayokuwa yanachezezwa katika uzito huu yatajulikana kama "Ubingwa wa IBF Africa wa Magoma Shaban".

IBF imeamua kuuita mkanda huu jina magoma Shabani ili kuweza kumuenzi na kuenzi mabondia wanaoleta mchango mkubwa
katika medani ya ngumi,ili  majina yao kubakia katika kumbukumbu
za michezo.
INNAILLAH WAINAILAH RAJIUN
habari kwa hisani ya Tone media/this day magazine
Categories:

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!