23 April 2012

Tangia binti huyu ashikiliwe kwa kuhusika na kifo cha msanii mwenzake hakuna siku niliyolia kama leo baada ya kuona hii picha.
Nimekivaa kiatu cha mama wa mtoto huyu anavyojisikia hasa kwa kumuona binti yake yupo katika ulinzi wa aina hii.
Ninasikika kuona binadamu wengine wapo mbele kumuhumu binti huyu kwa kumuita majina kibao,ni nani kati ya hao wanaomuita Elizabeth mzinifu ambae yeye hafanyi hiyo zinaa?Sikama ninashabikia hili ila tujifunze kuangalia tunayoyatenda sie kwanza kabla ya kumuhumu mwenzetu.
Pia inatupasa kujua na kufahamu kuwa lilomkuta huyu binti linaweza kumkuta mtu yoyote yule kama sio wewe bingwa wa kuhukumu basi hata mtoto wako au ndugu yako.
Sitaki kuzungumzi sheria yoyot hapa sababu mie sio mwana sheria,sitaki kuhukumu sababu mie sio mwenyezimungu,ila kikubwa ninakuombea mungu akuepushe na hili balaa mpz wangu.
Reactions:

0 comments:

Post a Comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!