22 June 2015


Bakwata leo uko wilayani Bagamoyo walikuwa kwenye mchakato wa kumpata mrithi wa kukaimu nafasi ya Muft/Sheikh Mkuu wa Tanzania.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Sheikh Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni, Mohamed Mhinga, alisema Baraza la Ulamaa litakaa na kuteua kiongozi atakayekaimu nafasi hiyo kwa muda siku 90 kabla ya kufanyika uchaguzi.

Na leo wametimiza ahadi hiyo kwa kumchaguwa Sheikh Abubakar Zubeir kukaimu nafasi hiyo ya Muft, atakaekaimu kwa muda wa siku 90 huku wakiendelea na utaratibu wa kufanya uchaguzi mkuu wa kumchagua Muft.

Uchaguzi huo utafanyika baada siku 90 kumalizika na fomu za kugombea zitatolewa kwa wagombea ambao watatoka miongoni mwa Baraza la Ulamaa ambao watachujwa mpaka kubaki mmoja.

MASHEIKH WA BAKWATA WENYE UWEZO NA WA KUMRITHI:
Baraza la Ulamaa ambalo ndilo litakalotoa Sheikh Mkuu mpya wa Tanzania linaundwa na Kadhi Mkuu, Sheikh Abdallah Mnyasi na manaibu wake, Sheikh Abubakar Zubeir na Sheikh Ali Muhidin Mkoyogole.

Wengine ni  Sheikh wa Mkoa wa Mwanza, Salum Fereji, Sheikh wa Mkoa wa Shinyanga, Ismail Makusanya, Sheikh wa Mkoa wa Kigoma, Hassan Kiburwa na Kadhi wa Mkoa wa Dar es Salaam, Hamid Masoud Jongo.

Sheikh Abubakar Zubeir, amechanguliwa leo uko wilayani Bagamoyo, atakaimu nafasi ya Muft Mkuu kwa siku tisini (90) kisha watapiga kura kumchagua nani anafaa kuchukuwa nafasi hiyo.

HABARI MPYA
Habari tulizozipata muda si mrefu zinasema kuwa "Mchakato wa kumpata Sheikh Mkuu utakamilika ndani ya siku saba (7) kuanzia sasa, wananchi na waumini wa dini ya kiislam na haswa wanachama wa BAKWATA wawe wavumilivu katika kipindi hiki," alisema Sheikh Lolila.

Katibu mkuu huyo hakutaka kuweka wazi sehemu wanapokutana wajumbe wa Baraza la Ulamaa ambao ndilo lenye mamlaka ya kumchagua kiongozi.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!