14 April 2012

Stage ya maharusi imependeza maishallah
  Vinywaji vikiingizwa katika mifuko ya plastic mmmmmh
Mwanakamati akiipanga vyema mifuko yenye vinywaji kwa ajili ya wageni waalikwa.
Vinywaji vikiwa tayari kwa ajili ya wageni waalikwa.lol
 Wageni waalikwa wakipita kujichukulia kimfuko chake vinywaji
 Wageni waalikwa na mifuko yao ya vinywaji

 Hii ni moja ya meza wazazi wao hawakupata bahati ya vifuko hahahaha
Hebu angali huu ukumbi ulivyopendeza jamani yaani kilichofanya uonekane mbaya ni hii mifuko ya plastic Aka Rambo.

Kwa mujibu wa mpiga picha nilikopata picha hizi, amesema kuwa vinywaji vimewekwa katika mifuko hii kutokana wageni waalikwa kuwa na tabia ya kuficha vinywaji katika handbag kubwa wanazobeba.
Hivyo kutokana na kuhusishwa kwa handbag katika hili,hapa inaonyesha ni kuwa wadada au wanawake ndio wezi wa vinywaji katika shughuli za watu,kwa kweli hii ni aibu kubwa.
Mie nilifikiri Pochi kubwa ni fashion kumbe zina kazi ya ziada kwa wanawake.
Au hii inatuthibitishia kuwa Mbeya wageni waalikwa huwa wanaiba sana vinywaji?
Swali hivi hawa wanakamati walishindwa kutafuta njia nyengine ya ugawaji wa vinywaji hadi waitie katika mifuko hii ya plastic au walikuwa na lengo la kuharibu picha za harusi za wenzao.
ninawaza tu bila ya kutoa sauti jamani sitaki chuki na mtu.

Picha kwa hisani ya
Reactions:

0 comments:

Post a comment

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!