SABABU.
UTI inasababishwa hasa na vimelea vya bacteria viitwavyo E.Coli,pia hata baadhi ya Virusi wanaweza kusababisha ungojwa huu.Kwa kawaida E.coli hawana madhara wanapokuwa katika mfumo wa chakula hasa katika utumbo mwembamba na mpana lakini wanapohamia katika mfumo wa mkojo wanakutana na mazingira tofauti na yale waliyoyazoea katika mfumo wa chakula.Hivyo katika juhudi zao kukabaliana na hali hiyo ya mazingira wanasababisha maambukizi katika mfumo(njia) wa mkojo.
DALILI ZA U.T.I
(MAAMBUKIZI KATIKA NJIA YA MKOJO)
1.Kwenda haja ndogo mara kwa mara dalili hii pia wanaweza kuwa nayo wenye kisukari.2.Kusikia maumivu wakati kwenda haja ndogo dalili hii pia wanaweza kuwa nayo wenye Kisonono- au Gono.
3.Maumivu ya tumbo hasa chini ya kitovu dalili nayo wanaweza kuwa nayo wenye PID.
4.Kuwa na homa kali hasa kwa watoto wadogo.
5.Kuwa na kichefuchefu na kukosa hamu ya kula.
0 comments:
Post a Comment