27 November 2014


Vitendo vya ukatili vilivyopamba moto hivi karibuni vya mashambulio ya hadharani dhidi ya wakina mama kwa misingi ya nguo walizovaa, Wakenya wanatoa wito kwa hatua kali kuchukuliwa katika kudhibiti unyanyasaji wa kijinsia, ambao umeenea licha ya jitihada za kutunga sheria za kulinda haki za akina mama.

Unyanyasaji wa kimwili na mhemko unaendelea kuwa kero, pamoja na unyanyasaji wa kijinsia ambao umeripotiwa mara nyingi, kwa mujibu wa Kituo cha Kusaidia uponyaji unaotokana na Vurugu za Kijinsia (GVRC) katika Hospitali ya Wakina mama, ambayo hutoa tiba na msaada kwa manusura wa unyanyasaji wa kingono na nyumbani.

"Kati ya 2011 na 2012, jumla ya matukio ya unyanyasaji wa kijinsia 2,532 na matukio mengine 422 ya unyanyasaji wa kimwili uliripotiwa," Mkurugenzi Mtendaji wa GVRC Alberta Wambua aliiambia Sabahi.

Katika asilimia 90 ya matukio yote yaliyoripotiwa ya unyanyasaji wa kijinsia, wanawake na wasichana walikuwa waathirika, alisema.

Kituo hicho kimefanya majumuisho ya matukio 1,864 yaliyoripotiwa ya unyanyasaji dhidi ya wakina mama kati ya Januari na Mei mwaka huu, kukiwa na asilimia 84 ya matukio ya unyanyasaji wa kingono na asilimia 16 ya unyanyasaji wa kimwili, Wambua alisema.

Januari, kituo hiki kinatarajia kutoa ripoti kamili yenye matukio yote yaliyoripotiwa kati ya 2013 na 2014. Wambua alisema idadi ya jumla hadi sasa inaonyesha ongezeko kubwa la unyanyasaji wa kimwili na kingono dhidi ya wanawake.

"Idadi tunayotoa inawasilisha sehemu tu ya matukio halisi yanayotokea na kuripotiwa katika nchi yote, ambayo inaonyesha wakina mama na wasichana wanapata shida kubwa ya maumivu na mateso," alisema, akiongezea kwamba jitihada za kuwafanya wanaume watambue uhalifu wa unyanyasaji kama huo unaopaswa kuongezwa.

Uvaaji wangu, uchaguzi wangu

Wambua alisema ameshtushwa na mashambulio ya hadharani yaliyoenea ya hivi karibuni dhidi ya wanawake.

Katika matukio mbalimbali, wanawake wamekuwa wakishambuliwa na kuvuliwa nguo kwa nguvu mtaani kwa sababu ya namna walivyovaa, alisema, ambayo ni ishara ya kutisha kwamba ghasia ya kijinsia kwa sasa inajumuisha mashambulizi ya kuvamia mbali na unyanyasaji wa nyumbani na mashambulio ya kingono.

Mamia ya waandamanaji walitembea Nairobi tarehe 17 Novemba kupinga shambulio la mwanamke aliyevuliwa na kundi baada ya kudai kuwa sketi yake ilikuwa ya kubana sana na fupi sana.

Siku moja kabla ya mkusanyiko huo mkubwa, polisi waliwakamata wanaume zaidi ya dazeni kuhusiana na kumfanyia mwanamke katika shambulio linalofanana na hilo katika kituo cha basi cha Nairobi.

Mashambulio mengine mawili kama hayo yameripotiwa huko Mombasa na Nairobi katika siku za karibuni, na yamesababisha kukamatwa kwa angalau polisi mmoja.

Matukio haya, ambayo yalitokea mchana kabisa, yamechochea hasira za wananchi kote nchini Kenya.

Wakenya wameitaka mitandao ya kijamii kulaani ukatili wa kijinsia na kutoa wito wa kuheshimu uhuru wa wanawake kwa kutumia alama ya #NguoYanguChaguoLangu, huku mjadala mkali ukiendelea kwa vikali katika vyombo vya habari.

Baada ya kuandamana kutoka Uhuru Park hadi kituo cha basi cha Embassava kwenye barabara ya Accra, eneo la moja ya mashambulio, waandamanaji hao walielekea kwenye ofisi ya Inspekta Jenerali wa Polisi David Kimaiyo kuwasilisha malalamiko yaliyotiwa saini.

Waandamanaji walitembea hadi Mahakama Kuu ya Kenya, ambako Mwanasheria Mkuu Willy Mutunga aliwapokea na kuahidi atawasilisha malalamiko kwenye Baraza la Taifa la Usimamizi wa Sheria, ambapo yeye ni mjumbe.

"Uvunjaji huu wa sheria ambapo tunawaona watu wakiwavamia wanawake ni kinyume na katiba," Mutunga alisema kwa kundi lililoshangilia. "Wanaume hao wanawapa wanaume wengine jina baya."

Wanawake wadai kupewa uhakika

Wale waliohudhuria mkutano huo, ambao uliandaliwa na kikundi cha Kilimani Mums, walilaani shambulio na kuiomba serikali kuwafikisha wakosaji katika vyombo vya sheria. Pia walidai kwamba viongozi wa kisiasa walaani hadharani matukio hayo na kuwahakikishia wanawake usalama wao.

"Ukweli kwamba shambulio la kutisha lilitokea mchana kweupe kwenye mtaa wenye shughuli nyingi katika mji mkuu bado hakukuwa na [ofisa] wa polisi hata mmoja katika eneo ili kusaidia wanawake walionyanyaswa kimwili na kihisia kunaacha maswali mengi kuhusiana na hali ya polisi yetu," alisema Koki Gatabaki, mwenye miaka 29, muigizaji anayekua.

Ukiukaji huo unapunguza mafanikio ambayo Kenya imeyapata katika kuhakikisha haki sawa kwa wanawake, aliiambia Sabahi. "Inasikitisha, matukio kama hayo yanatokea kwa sababu ya wachache ambao wanafanya uhalifu hawaadhibiwi."

Matukio ya hivi karibuni ya unyanyasaji na ukatili yana athari kubwa kwa kuwa ni "ishara ya uvunjaji wa sheria na kukosa uvumilivu katika nchi," alisema wakili mstaafu wa mahakama kuu Kariuki Muthe'ngi, mwenye miaka 65.

Katiba ya Kenya na mswada wa haki unahakikisha kwa uwazi haki za wanawake, alisema.

"Sheria ni kali lakini utekelezaji ni dhaifu au haupo kwa sababu vyombo vya kutekeleza sheria viko katika usingizi mzito na vinachukua hatua pale tu wakati hali haivumiliki baada ya maandamano au wakati wanapoagizwa na viongozi wa serikali," aliiambia Sabahi.

"Mfumo wa Sheria za Jinai nchini Kenya haujawezeshwa vya kutosha kuwalinda wanawake na ukatili wa kijinsia licha ya Sheria ya Makosa ya Kubaka ya mwaka 2006 iliyotungwa na bunge kwa sababu inakosa utekelezaji na utaratibu wa ufuatiliaji wa vyombo husika vya serikali ili kuhakikisha ufuataji wa sheria na katiba," alisema.

Wachunguzi wa polisi na waendesha mashtaka pia wanakosa mafunzo maalumu kuhusu utoaji wa Sheria ya Makosa ya Ngono, ambayo ni mojawapo ya sababu kuu inayochangia kiwango kikubwa cha kuachiwa huru katika kesi hizo wanaporipotiwa, aliongeza.

Ghasia ya kingono na kijinsia inatakiwa kusimamiwa na wanasheria wazoefu tu na sio waendesha mashtaka wa polisi, alisema, akiongeza kwamba polisi kwa sasa wanasimamia kesi hizi katika mahakama zilizo chini yao, ambazo zinafafanua kwa nini nyingi miongoni mwao zinatupwa nje na washukiwa kuachiwa huru.

Mkuu wa Idara ya Uchunguzi wa Makosa ya Jinai huko Nairobi Nicholas Kamwende aliiambia Sabahi kwamba kikosi kilichobobea cha polisi cha "kuzuia uvuaji nguo" kiliundwa kushughulikia kuibuka kwa mashambulio dhidi ya wanawake.

Alisema inspekta Jenerali wa polisi amechagua dazeni za wanawake kufanya kazi kwa kificho katika vituo vya mabasi na maeneo mengine ya umma na amewawezesha kwa rasilimalii zote zinazotakiwa kufanya kazi hiyo.

Kamwende pia aliwatia moyo wanawake ambao walikuwa waathirika wa mashambulio hayo kujitokeza katika kituo chochote cha polisi ili kuandikisha maelezo, ambayo yatasaidia katika uchunguzi na kukamatwa kwa wahalifu. Alisema polisii watachukulia taarifa yoyote inayotolewa kuwa siri.

Viongozi wa dini wazungumza

Kuibuka kwa ukatili dhidi ya wanawake ni suala kubwa na viongozi wa dini wanapaswa kujiandaa vizuri kushughulikia tatizo hilo, alisema Askofu Mark Kariuki, mchungaji mkuu wa Kanisa la Deliverance lililopo Nairobi.

Kariuki alitoa wito kwa Wakenya wote, akianza na viongozi wa kanisa, kutumia tukio la hivi karibuni la ukatili wa kijinsia kama kichocheo cha kuanza kuzungumza na kuzuia "uelewa wa ukatili wa kingono na wa majumbani ulioenea katika mikusanyiko yao."

"Kwa amani iliyopo ya jamii, utatuzi wa matukio ya ukatili wa kijinsia ni kushughulika na wanaume na wavulana kama washirika dhidi ya hilo," aliiambia Sabahi, akiongeza kwamba viongozi wa serikali na wa dini wanapaswa kushirikiana kuendesha kampeni za kuzuia ukatili kwa kuwalenga wanaume.

Mchungaji Murungi Igweta wa Kanisa la Trinity Baptist huko Nairobi aliunga mkono, akisema ukatili dhidi ya wanawake "unazuia mchango wao katika maendeleo ya taifa na hali nzuri ya familia zao."

Alisema ilikuwa bahati mbaya kwamba baadhi ya wanawake hawaungwi mkono katika makanisa yao wanapotafuta talaka au kutengana kutokana na hali ya kunyanyaswa kimwili. "Inaweza hata kuwa hali mbaya zaidi katika matukio ambapo mwatirika anatengwa na kanisa katika mazingira hayohayo," aliiambia Sabahi.

"Ukatili dhidi ya wanawake unapaswa kushughulikiwa kiundani katika kanisa na wanaume waliohusika," alisema.

Wale wanaofanya ghasia dhidi ya wanawake wanapaswa kuaibishwa katika jamii zao na kuadhibiwa katika mfumo wa kisheria, alisema Mohamud Abdilahi, imamu wa Msikiti wa Amani ulioko Mombasa.

Pamoja na kuwa tukio la uvuaji nguo linaweza kuzaa uovu, alisema, hii bado sio utetezi wa kufanya ukatili wa kimwili, na mwathirika hapaswi kulaumiwa kwa shambulio hilo.

"Ukatili dhidi ya wanawake unaendelea kuwepo kwasababu ya wanaume katika jamii ambao wanafanya ukatili na hawawajibishwi," aliiambia Sabahi, akitoa wito wa adhabu kali zaidi na utekelezaji mzuri wa sheria kama kizuizi.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!