11 February 2013






Ilikuwa ni mida ya adhuhuri, nilipokuwa kwenye miangaiko yangu ya hapa na pale, ndipo nilipokutana na waandamaji na wanaharakati wa jiji la Cork, wakipinga aina mpya ya kodi ya majengo kwa jina la "Property Tax"

Hii ni kodi mpya kwa nchi nzima ya Ireland, ikiwataka kwa kila mtu ambaye anamiliki nyumba zaidi ya moja basi kulipa kodi hii. Mahijiano ya mmoja wa wanaharakati kiongozi (Karen Doyle) wa hayo maandamano alikuwa na haya ya kusema

 "The Government are manipulating language - this is not a real property tax, it is a tax on our homes. And there is nothing “progressive” about it. Council services will not improve as a result of it - in fact, they will be cut further in the next few years. Instead, it is a smash and grab raid to pay for the bank bailouts and to give the bondholders their pound of flesh. "We object to the 'choice' about to be 'offered' to us by the Government - sign up for the tax or have it deducted from your wages or social welfare. This is blatant robbery and we intend to resist it..."

Hayo ndio yalikuwa baadhi ya malalamiko ya Mwanaharakati huyo Karen Doyle, akiwataka wananchi wasijiandikishe kulipa, maana aina hii ya kodi ni wizi na aina faida yoyote kwani kuna uwezekano wa hii kodi kuongezeka miaka ijayo na kuzidi kumkandamiza mlalahoi wa Ireland.

0 comments:

Post a Comment

.

Subscribe to RSS Feed Follow me on Twitter!